Saturday, December 5, 2020

Mshindi wa Vodacom Shangwe Shangwena akabidhiwa gari yake mjini Biharamulo

Mkuu wa Mauzo, Vodacom Tanzania Plc Kanda ya Ziwa, Ayubu Kalufya (kulia) akimkabidhi funguo mshindi wa kwanza wa bahati nasibu ya promosheni ya Vodacom Shangwe Shangwena, Bi. Happiness Manembe Apollo ambaye ni mkazi wa Biharamulo aliyejishindia gari jipya aina ya Renault KWID. Promosheni hiyo itawezesha watumiaji wa M-Pesa kujishindia magari mapya 5 pamoja na zawadi kemkem zenye thamani ya zaidi ya shilingi 5 bilioni, unachotakiwa kufanya ni kutumia huduma ya M-Pesa kadri uwezavyo katika msimu huu wa sikukuu. Jumla ya magari matano, pesa taslimu shilingi milioni 25 na zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi 3 bilioni kutolewa ndani ya wiki 5

Meneja Masoko wa Vodacom Tanzania PLC, Grace Kijo (kulia) akimkabidhi mshindi wa kwanza wa promosheni ya Shangwe Shangwena, Bi. Happiness Manembe Apollo fulana mara baada ya kuzawadiwa gari aina ya Renault KWID.

Sehemu ya umati uliojitokeza kwenye hafla ya makabidhiano ya gari kwa mshindi wa promosheni ya Shangwe Shangwena iliyofanyika stendi ya mabasi mjini Biharamulo

 

No comments :

Post a Comment