Sunday, December 6, 2020

MHANDISI NYAMHANGA ATOA MIEZI MITATU KUKAMILIKA KWA JENGO LA UPASUAJI KILOLO

…………………………………………………………………………………….

Na. Angela Msimbira IRINGA

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga ametoa miezi mitatu kwa Mkandarasi PACHA Building construction kukamilisha ujenzi wa

Jengo la Upasuaji ifikapo Februari, 2021

Mhandisi Nyamhanga ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya hiyo Mkoani Iringa.

Amesema kuwa Hospitali hiyo kwa sasa imekamilika na imeanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje, lakini bado kuna baadhi ya majengo ambayo ujenzi wake haujakamilika jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za Serikali za kuhakikisha huduma zote za afya zinapatikana karibu na wananchi

Akifafanua zaidi amesema kuwa mkadarasi huyo aliwasilisha hati za malipo tatu na tayari Serikali ilishalipa hati mbili, hivyo anawajibu wa kuhakikisha Jengo hilo linakamilika kwa wakati uliopangwa ili lianze kutoa huduma kwa jamii.

“Hakuna sababu ya mkandarasi kusimamisha ujenzi, kwa kuwa serikali imeshalipa baadhi ya fedha, naagiza mkandarasi Pacha Buildingi Construction kuhakikisha anamaliza ujenzi ili wananchi wa Kilolo waweze kupata huduma ya upasuaji katika Hospitali hiyo” amesisitiza Mhandisi Nyamhanga

Wakati huo Mhandisi Nyamhanga Aidha. ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kuhakikisha wanasimamia kikamilifu ujenzi wa majengo yaliyobaki katika Hospitali ya Wilaya ya Kilolo ili iweze kutoa huduma kwa jamii.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kituo hicho Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Dkt Mohamed Manguna amesema mradi umegarimu zaidi ya shilingi bilioni 4.3 ambapo Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 4, wadau wa maendeleo shilingi milioni 37 na zaidi ya shilingi milioni 336 zimetolewa na Halmashauri hiyo kutoka katika mapato ya ndani.

Aidha, Dkt. Manguna amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali hiyo kutawezesha Halmashauri kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza, kupunguza kiwango cha magonjwa na vifo vya watoto wachanga na vifo vya mama wajawazito kupunguza uhitaji mkubwa wa huduma za rufaa hasa kwa akinamama wajawazito na watoto na kukabiliana na uhitaji mkubwa wa huduma za dharura za upasuaji Mkubwa na mdogo unaotokana na ajali za vyombo vya moto.

 

No comments :

Post a Comment