Kampuni
ya STAMIGOLD ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Madini la Taifa
(STAMICO) kupitia mgodi wake wa Stamigold Biharamulo (Stamigold
Biharamulo Mine - SBM) uliopo wilayani Biharamulo mkoa wa Kagera
umeshiriki katika Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoa wa
Shinyanga yaliyofanyika katika eneo la Butulwa Old Shinyanga Mkoani
Shinyanga.
Kilele cha Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini yaliyoongozwa na kauli mbiu ya ‘Biashara na madini ni chachu ya maendeleo Shinyanga’ kimefanyika Disemba 1,2020 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kikula.
Akizungumza
kwenye maonesho hayo, Meneja Mkuu wa mgodi Stamigold Biharamulo
Mhandisi Gilay Shamika, alisema mgodi huo unakabiliwa na gharama kubwa
ya uzalishaji wa madini ya dhahabu hivyo kuishukuru serikali kwa
kuwaunganishia huduma ya umeme kutoka Kituo cha Geita na hatua
iliyofikiwa ,inatarajiwa umeme kuanza kutumika Februari 2021 ambapo
kwasasa Mgodi unatumia genereta za dizeli.
"Tangu
mgodi huu uwe chini ya Serikali mwaka (2014), na kuanza uzalishaji
rasmi 2015, umekuwa ukiingia kwenye gharama kubwa ya kutumia Genereta na
mafuta ya Diesel yenye gharama za Shilingi Bilioni 1.2 kwa mwezi na
endapo tutapata huduma ya umeme gharama itapungua na tutatumia shilingi
Milioni 300",aliongeza Meneja Mkuu wa Mgodi , Mhandisi Gilay Shamika.
Hata
hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Prof. Idris Kikula akiwa
kwenye Banda la Mgodi wa StamiGold Biharamulo, aliupongeza mgodi huo kwa
kufufuka tena na kuanza uzalishaji wa madini akieleza kuwa faida
imekuwa ikipanda kila Mwaka na kusaidia STAMICO kulipa gawio Serikalini.
Kulia
ni Meneja wa mgodi Stamigold Biharamulo Mhandisi Gilay Shamika,
akimuelezea Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris
Kakula (katikati aliyevaa miwani) namna mgodi huo unazalisha madini ya
dhahabu alipotembelea Banda la Stamigold kwenye Maonesho ya Biashara na
Teknolojia ya Madini eneo la Butulwa Old Shinyanga mkoani Shinyanga
Disemba 1,2020. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kushoto
ni Meneja wa mgodi Stamigold Biharamulo Mhandisi Gilay Shamika,
akimuelezea Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris
Kakula (wa pili kulia) namna mgodi huo unazalisha madini ya dhahabu
alipotembelea Banda la Stamigold kwenye Maonesho ya Biashara na
Teknolojia ya Madini eneo la Butulwa Old Shinyanga mkoani Shinyanga
Meneja
wa mgodi Stamigold Biharamulo Mhandisi Gilay Shamika, akimuelezea
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula (wa pili
kulia) namna mgodi huo unazalisha madini ya dhahabu
Kulia
ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Prof. Idris Kikula akizungumza
kwenye Banda la Mgodi wa StamiGold Biharamulo, na kuupongeza mgodi huo
kwa uzalishaji wa madini wakati wa maonesho ya Biashara na Teknolojia ya
Madini mkoa wa Shinyanga Disemba 1,2020.
Kulia
ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Prof. Idris Kikula akizungumza
kwenye Banda la Mgodi wa StamiGold Biharamulo, na kuupongeza mgodi huo
kwa uzalishaji wa madini wakati wa maonesho ya Biashara na Teknolojia ya
Madini mkoa wa Shinyanga Disemba 1,2020
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments :
Post a Comment