**************************************************
Na Woinde Shizza,Arusha.
Askari polisi watatu
na raia sita akiwepo mfanyabiashara wa madini Lucas Mdeme,
wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Arusha, kwa tuhuma za kumteka
na kumuomba rushwa n Mwenyekiti wa chama cha wauzaji wa madini
Tanzania(TAMIDA) Sammy Mollel .
Akizungumza na
waandishi wa habari, Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Salum
Hamduni,alisema tukio hilo limetokea Desemba 14,mwaka huu na kuwataja
waliokamatwa ni Askari namba H.125 Gasper Paul kitengo cha
Intelijensia Makao makuu ya Polisi Dodoma.
Wengine ni Askari
namba G 5134 DC Heavenlight Mushi wa kitengo cha Intelijensa Mkoa wa
Kinondoni na Askari namba H.1021PC Bryton Murumbe kutoka Dodoma.
Kamanda Hamduni
aliwataja wengine waliokamatwa ni pamoja na Mfanyabiashara wa
madini,Lucas Michael Mdeme(46) ambaye ni meneja kampuni ya kuuza madini
ya CROWN Lapidary Ltd yajijini Arusha,Shabani Benson(49)
mfanyabiashara wa dodoma na Nelson Lyimo(58) mfanyabiashara wa
Kimandolu Arusha.
Watuhumiwa wengine
ni Leonia Joseph(40) Sekretari wa kampuni ya Germs & Rocks
Ventures,Omary Mario(43)mfanyaviashara wa eneo la Olorieni Arusha na
Joseph Chacha(43) mfanyabiashara wa Elboru Arusha.
Alisema awali polisi
iliwakamata watuhumiwa watatu, wakiwepo polisi wawili DC Muchi,PC
Murumbe na mfanyabiashara Benson ofisi ya Germs & Rocks baada ya
kuenda kushawishi na kupokea rushwa na baadaye kukamatwa watuhumiwa
wengine sita
Alisema taarifa za
awali zinadai kuwa watuhumiwa hao, waliomba rushwa ya sh 30 milioni na
walipokea tayari fedha sh 10milioni na kisia kilichobaki walipofuata
ndio walikamatwa.
Mollel alikiri
kukamatwa na watuhumiwa hao, ambao walikuwa na silaha na kuondoka nae
kuelekea Dodoma na wakiwa njiani kabla ya kufika Dodoma ndipo waliomba
fedha .
Hata hivyo, alisema kwa sasa hawezi kufafanua zaidi tukio hilo, kwani bado uchunguzi unaendelea na watuhumiwa bado wanakamatwa.
“Huu ni mtandao mkubwa wametapeli wafanyabiashara kadhaa hivyo vyombo vya usalama vinafayakazi”alisema
Mmoja wa watuhumiwa
hao,Mdeme ambaye pia ni mmoja wa viongozi wa TAMIDA na meneja wa kampuni
anayofanyakazi ya Crown Lapidary ltd iliwahi kutajwa katika kesi ya
Utoroshaji madini katika uwanja wa kimatataifa wa kilimanjaro.
Mfanyabiashara
mwenye asili ya kiasia,Raia wa India, Anarag Jain(44) akitorosha madini
gramu 2015.59 yenye thamani ya dola 310,137.255 (Sawa na Sh 670
milioni).
Baada ya kukamatwa
na madini kutaifishwa mbele ya hakimu Mfawidhi wa mahakama ya mkoa
Kilimanjaro, Joachim Tiganga iliitaja kampuni ya Crown Lapidey
inayomilikiwa na Raia wa Kenya,Rajan Verma kuwa ndio ambao walihusika
kumuuzia mfanyabiashara huyo madini na kuahidi kumsadia kutorosha.
Mdeme alitajwa
mahakamani kuhusika kuwarubuni maafisa wa usalama wa uwanja huo na
wafanyakazi, Askari E.3985D/CPL Endrew ,Caphace Rangia ,Rachel Shao, na
Debora Komba kumuingiza ndani ya uwanja huo lakini baadaye madini
yalikamatwa.
Watuhumiwa ha wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
No comments :
Post a Comment