KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Kessy Maduka,akikagua banda ya wanawake wajasiriamali kabla ya kuwahutubia wananchi waliofika katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) jijini Dodoma.
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Kessy Maduka,akiwahutubia wananchi waliofika katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) jijini Dodoma.
Baadhi ya wananchi wakifatilia hotuba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Kessy Maduka,wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) jijini Dodoma.
Sehemu ya wanafunzi wakifatilia maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) jijini Dodoma.
Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii jiji la Dodoma Bi.Sharifa Nabalaganya,akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) jijini Dodoma.
Baadhi ya vijana wakionyesha ubora wao wa maigizo wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) jijini Dodoma.
Mratibu wa Ukimwi Dodoma Abdul Ahmed ,akitoa taarifa juu ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na wanaojua hali zao wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya siku ya UKIMWI Duniani kwa Mkoa wa Dodoma Crispin Kapinga akitoa neno la shukrani wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) jijini Dodoma.
………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Dodoma Kessy Maduka amesema kuwa kuna haja ya kuweka
mikakati ya kuitoa Dodoma kwenye kundi la Mikoa yenye maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi ambayo kwa sasa yapo kwa asilimia 5 kutoka asilimia 2.9 kwa mwaka 2013/2014.Takwimu hizo ni kwa mujibu wa utafiti wa Tanzania health impact survey (This)unaofanyika kwenye kaya kila baada ya miaka mitano ambao umeonyesha uwepo wa ongezeko la asilimia 2.1.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Nyerere Square) Maduka amesema kuwa eneo ambalo limeonekana kuwa na maambukizi mengi mapya ni kundi la vijana.
Aidha Maduka amesema kuwa kundi la Vijana kuanzia umri wa miaka 15 hadi umri wa miaka 24 ndilo kundi linalopata maambukizi kwa kasi kubwa nchini.
“Miaka ya nyuma tumeona tulikuwa kwenye mikoa yenye maambukizi kidogo ya Ukimwi lakini sasa tupo kwenye mikoa hatarishi,hapa ni lazima tuweke mikakati ya kupamba nayo kwa pamoja,Dodoma kamwe haiwezi kukubali hali hii,”amesema Maduka
Aidha ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma katika siku hiyo kujitokeza kwa wingi kwakupima na kutambua afya zao Mapema na kuacha uoga wa kujua afya zao kuwa kigezo cha kuhofia kufa Mapema.
” Kila mmoja wetu ampime atambue afya yake kwani ukipima na ukijitambua Mapema kama unamaambukizi ya virus vya Ukimwi unanafasi ya kuishi vizuri kea amani na furaha,” amesema.
Naye Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii jiji la Dodoma Bi.Sharifa Nabalaganya amesema kuwa unyanyasaji wa kijinsia umekuwa kisababishi kimojawapo cha kupata maambukizi mapya ya virusi hivyo.
“Niwaombe vijana mjitambue Ili mfikie malengo yenu,nina imani kila mmoja akitimiza jukumu lake tutaweza kutokomeza maambukizi haya,”amesisitiza
Awali Mratibu wa Ukimwi Dodoma Abdul Ahmed amesema kuwa makisio ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na wanaojua hali zao kwa Mkoa 55,133 ambapo kufikia mwezi Septemba Mwaka huu walishawafikia watu 35,064 sawa na asilimia 71.
“Kati ya idadi hiyo ya watu tuliowafikia asilimia 99.5 tumewaunganisha katika huduma za tiba na matunzo ambapo kati yao asilimia 85 wamefanikiwa kufubaza virusi hivyo,”amesema Ahmed.
Hata ametaja baadhi ya changamoto zilizopo katika mapambano dhidi ya virusi hivyo kuwa ni uwepo wa unyanyapaa na idadi ndogo ya wanaume wanaojitokeza kupima afya zao.
Naye Anamary Oscar akisoma risala ya waathirika wa virusi hivyo ametoa ombi la eneo la kufanya ujasiriamali na kuwataka vijana kujiunga kwenye vikundi ili waweze kukopesheka.
“Katika mapambano ya virusi hivi tunakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo gharama za kuwafuatilia walioacha matumizi ya dawa ili tuweze kuwarejesha kwenye utaratibu wa matibabu,”amesema
Kauli mbiu ya siku ya Ukimwi duniani Mwaka huu inasema mshikamano ws kimataifa tuwajibike pamoja.
No comments :
Post a Comment