Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika mahafali ya 50 ya
chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Mabalozi
wanaowakilisha nchi zao hapa Nchini wakifuatilia sherehe za mahafali ya
50 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wahitimu wa Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa ukumbini tayari kwa ajili ya kutunukiwa
shahada katika mahafali ya 50 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es
Salaam
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akimtunuku shahada ya heshima Naibu Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Namibia
ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akimkabidhi moja kati ya zawadi Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Namibia
ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtunuku shahada ya heshima Dkt. Pius Msekwa katika mahafali ya 50 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi moja kati ya zawadi SPIKA wa Bunge
Mstaafu, Dkt. Pius Msekwa katika mahafali ya 50 ya chuo hicho
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
akiwasilisha salamu za Serikali kwenye mahafali ya 50 ya chuo hicho
yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)
akimkabidhi zawadi ya vitabu Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Namibia
ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akipata picha ya pamoja na Spika wa Bunge Mstaafu, Dkt. Pius
Msekwa,Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Namibia ambaye pia ni Waziri wa
Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe. Netumbo Ndaitwah,Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi,Makamu Mkuu
wa Chuo hicho Profesa William Anangisye pamoja na viongozi wengine
katika mahafali ya 50 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
*************************************
Spika wa Bunge
Mstaafu, Dkt. Pius Msekwa, amesema shabaha ya elimu ya juu katika maisha
ya sasa ni kumkomboa binadamu kifikra na kumpa uwezo wa kujisimamia,
sio kuajiriwa na Serikali kama inavyodhaniwa na wengi.
Amesema kulingana na
tafsiri hiyo ni muhimu wahitimu wakaondoa fikra na mitazamo ya kuajiriwa
na serikali na badala yake wajiandae kuitumikia nchi kwa namna yoyote
halali watakayobuni wenyewe.
Dkt. Msekwa,
aliyasema hayo baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa
Sheria, wakati wa hafla ya Mahafali ya 50 duru ya tatu ya Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam tawi la Mwalimu Nyerere.
Alisema awali tafsiri ya elimu ilikuwa ni kuajiriwa na serikali na hata mfumo wa mafunzo ulifanyika kufanikisha hilo.
Dkt. Msekwa, alisema
kwa wakati huo hata majukumu ya Chuo Kikuu yalikuwa ni kuandaa wataalamu
kwa ajili ya utumishi wa umma na idara nyingine za serikali.
Aliongeza kuwa hata idadi ya wanafunzi waliodahiliwa ilifanyika kulingana na mahitaji ya watumishi tu.
“Wakati huo kusoma
chuo kikuu ilikuwa haki ya wateule wachache kwa ajili ya kuitumikia
serikali na idara nyingine za umma,” alisema.
Kulingana na Dkt. Msekwa, wahitimu wakati huo walikuwa na uhakika wa ajira.
Alisema hayo
yalibadilika baada ya kufanyika kwa mabadiliko ya sera kutoka elimu kuwa
haki ya wateule wachache na kuwa haki ya watu wote.
“Hii ilibadili
majukumu ya vyuo vyetu, kutoka kutoa elimu kwa waajiriwa hadi kutoa
elimu ya kuwakomboa fikra na tafsiri hiyo ndiyo iliyotumika wakati wa
Azimio la Arusha na ikazaa neno ‘Elimu ya Kujitegemea’, ” alisema.
Alitaka wahitimu kujiandaa kifikra katika uhalisia wa tafsiri ya elimu kwa sasa na waondokane na mitazamo ya kuajiriwa.
Kwa upande wake
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa
Palamagamba Kabudi, alisema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
kinatarajiwa kupokea Dola milioni moja kila mwaka kwa miaka 10 kutoka
Kampuni ya Barrick Ltd, kwa lengo la kuendeleza kitivo cha Madini
kilichoanzishwa chuoni hapo.
Alisema hatua hiyo ni
kulingana na baadhi ya vipengele vya mkataba Kati ya serikali na
Kampuni hiyo ambapo UDSM itakuwa ikipewa Dola milioni moja kila mwaka
kwa kipindi cha miaka 10.
“Hii tumelenga
ikatumike kuboresha taaluma ya madini inayotolewa katika chuo kikuu cha
Dar es Salaam, ukizingatia hii ni miongoni mwa taaluma mpya
zilizoanzishwa chuoni hapa,” alisema.
Nae Makamu Mkuu wa
Chuo hicho Profesa William Anangisye, alisema hiyo ni mahafali ya 50
kufanyika tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Alisema chuo hicho kitaendelea kushirikiana na TAASISI nyingine za kimataifa katika kuboresha utoaji wa taaluma.
Prof. Anangisye
Alitaka miongoni mwa mafanikio ealiyopitia chuoni hapo ni pamoja na
kuongezeka kwa bajeti ya utafiti kutoka sh. bilioni 1.4 mwaka 2019 hadi
sh. bilioni 1.9 mwaka huu.
Pia alisema katika
mahafali hiyo wameamua kuwatunuku shahada za heshima za Udaktari Pius
Msekwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Netumbo Ndaitwa, ikiwa no
ishara ya kutambua mchango wao katika mapambano ya mambo mbalimbali
ikiwemo Diplomasia, Uhuru na utumishi uliotukuka.
No comments :
Post a Comment