Monday, November 16, 2020

Waziri Mkuu wa Uingereza ajitenga tena baada ya kukutana na mtu mwenye corona


 Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza kujitenga baada ya kukutana na Mbunge wa Ashfield, Lee Anderson ambaye baadaye alithibitishwa kuwa na Virusi vya Corona.

Johnson amesema, alitafutwa na Mamlaka na kutakiwa kufanya hivyo kama taratibu zinavyoelekeza, japokuwa hana dalili zozote za COVID19 baada ya kuwa karibu na Anderson kwa takriban dakika 35.

Mwezi Aprili, Waziri huyo aligundulika na Ugonjwa huo na kulazwa ICU kwa siku 3. Hadi sasa Uingereza imerekodi visa 1,369,318 na vifo 51,934.

 

No comments :

Post a Comment