Wednesday, November 18, 2020

WATAKIWA KUACHA KUTOA DAWA KWA MGONJWA ASIYE NA CHETI CHA DAKTARI


Mganga Mkuu wa serikali Profesa Abel Makubi akizungumza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya kuamasisha wananchi kuhusu uelewa wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa aina ya Antibayotiki uliofanyika kwenye hoteli ya New Afrika leo jijini Dar es salaam.

Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya kuamasisha wananchi kuhusu uelewa wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa aina ya Antibayotiki uliofanyika kwenye hoteli ya New Afrika leo jijini Dar es salaam.

Mfamasia Mkuu wa serikali Daud Msasi akitoa ufafanuazi wa mambo kadhaa katika uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya New Afrika jijini Dar es salaam.

Gibons Andrew Kayuni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Mifugo Wizara ya Mifugo na Uvuvi akifafanua jambo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika uzinduzi huo.

Baadhi ya wataalam na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria katika uzinduzi huo.

Mganga Mkuu wa serikali Profesa Abel Makubi akizungumza na Mfamasia Mkuu wa serikali Daud Msasi kutoka kulia ni 

Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Afya , Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya wanawake,Wazee na Watoto Catherine Sungura na  Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma,wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA),Gaudensia Simwanza.

Baadhi ya wataalamu na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria katika uzinduzi huo.

Baadhi ya wataalam kutoka taasisi mbalimbali  waliohudhuria katika uzinduzi huo.

……………………………………………………………..

SERIKALI imewataka wamiliki wa maduka ya dawa za binadamu kuacha kutoa dawa kwa

mgonjwa ambaye hana cheti cha daktari/tabibu kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria zilizowekwa.

Pia imewaomba wananchi kuhakikisha watumia dawa kwa uangalifu na umakini zaidi ili kuweza kuepuka usugu wa vimelea dhidi ya dawa aina ya Antibayotiki.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam leo na Mganga Mkuu wa serikali Profesa Abel Makubi alipokuwa akizindua maadhimisho ya wiki ya kuamasisha wananchi kuhusu uelewa wa usugu wa vimelea dhidi ya dawa aina ya Antibayotiki

Alisema baadhi ya maduka ya dawa yamekuwa yakifanya makosa kwa kumpatia mgonjwa dawa bila ya kuona cheti kilichotolewa na daktari.

“Cheti cha daktari ni muhimu kwa mgonjwa kuwanacho kabla kupewa dawa ya aina yoyote iwe katika kituo cha huduma ya afya au duka la dawa”alisema Profesa Makubi

Alisema kutolewa kwa dawa hizo kiolela bila ya kuona cheti cha daktari kinaweza kumsabisha mgonjwa usugu wa vimelea vya dawa.

Alisisitiza kuwa uwepo wa usugu wa vimelea vya katika dawa Antibayotiki unaweza kuliweka taifa katika kupoteza nguvu kazi pamoja na kutumia fedha nyingi kutumia kununua dawa

Profesa Makubi alisema kutokana na matumizi mabaya ya dawa hizo kwa tiba ya binadamu na wanyama madhara yake yamekuwa makubwa ya kutisha.

Alisema kwa mujibu wa tafiti zimeonesha kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa za matumizi ya dawa hizo kutumika isivyo sahihi.

” Asilimia 50 ya dawa zimekuwa zikitumika isivyo sahihi huku matumizi makubwa kutibia mifugo na kuchaganywa katika vyakula vya wanyama kinyume na taratibu za kitabibu”alisema Profesa Makubi

Aliongeza kuwa ripoti ya benki ya dunia ya mwaka 2017 inabainisha kuwa zaidi ya watu laki 7 wanafariki Kila mwaka kutokana na usugu wa dawa hizi.

Akizungumza kuhusu utumiaji wa dawa kwa mgonjwa alisema anapaswa kufuata maelekezo ya dawa sahihi ikiwa ni pamoja na kuepuka kukatisha dozi.

” Kila mtu anapaswa kufuata matumizi sahihi ya dawa ikiwa ni pamoja na kutozitumia kiolela ikiwa ni pamoja na kutokukatisha dozi “alisema Profesa Makubi

Kwa upande wake Mfamasia Mkuu wa serikali Daud Msasi alisema kwa sasa wanafanya utaratibu wa kupitia maduka yote Kama njia ya kujiridhisha katika utoaji wa dawa.

Aidha alitaka jamii kuacha kutumia dawa ambazo mtu tayari amezitumia kwani kufanya hivyo kinaweza kusababisha usugu wa dawa.

Pia alisema kupitia wiki hii wanaendelea kutoa elimu ya uelewa juu ya matumizi sahihi ya dawa aina ya Antibayotiki ili siweze kusababisha vimelea vya usugu dhidi ya dawa hizo.

 

No comments :

Post a Comment