Wednesday, November 25, 2020

WAKANDALASI MKOANI KIGOMA WATAHADHARISHWA.

**************************************

Na Rahel Nyabali Kigoma.

Serikali ya mkoa wa kigoma imeitaka  mamlaka ya maji mjini na vijijini  RUWASA kuhakikisha 

inakamilisha kwa ubora sitahiki   miradi ya maji katika vijiji ishirini na mbili .

Akizindua miradi hiyo ya maji mkuu wa mkoa wa kigoma Tobius Ndengenye  wilayani Buhigwe ,amesema miradi  inaogharimu kiasi cha  zaidi shiringi  bilioni 20  kwa mkoa mzima ambao miradi hiyo imefadhiliwa  na Serekali ya Ubirigiji kwa Ushilikiana Serekaliya Tanzania na kusisitiza  kukamilika kwa mradi mapema ili wanchi waondokane na adha ya maji.

 Mhandisi wa maji Ruwasa mkoani kigoma Matias Mwenda ameahidi kusimamia kikamilifu ma kumtaka mkandarasi wa Kampuni ya Seregeti limited kukamilisha kwa  kwa wakati .

Mkuu wa wilaya ya buhigwe Kanali Michael Ngayalina amewasisitiza wananchi kutunza miundombinu ya maji kwani miradi mingi katika maeneo mbalimbali imekuwa  ikitumika kwa mda mfupi kasha kuharibika.

Hatahivyo wananchi walio pata miradi hiyo  akiwemo Tamasha Athumani na Adamu  Makuka wameshukuru Serekali kwa kuwaletea miradi hiyo na kuahidi kulinda miundombinu ya miradi ya maji.

 

No comments :

Post a Comment