Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
ILI
kuhakikisha soko la Utalii kwa nchi za Afrika liwezekukua latakiwa kuwa
na kiwango cha fedha za utalii kwa Afrika nzima (African Rates) ambazo
zitasaidia waafrika kutembelea vivutio vilivyopo barani.
Hayo
aliyasema Mkurugenzi wa Msafiri Travel, Leina lemomo wakati
akizunngumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Alisema kuwa
bara la Afrika nalo linawatalii wengi lakini tatizo ni kuwa na viwango
tofauti kwa vya kuingilia katika sehemu za vivutio vilivyomo barani.
“Afrika
kama bara na Tanzania kama Nchi hatujawahi kuangalia utalii wa ndani
lakini kwa miaka mingi ambapo utalii unaendelea hatujawahi kuwa na
kiwango cha Fedha (African Rates)au gharama ambazo zinavutia waafrika
kutoka bara nzima la Afrika."
Ukiangalia
kwenye soko la Utalii unaona kuna viwango tofauti tofauti ambavyo ni
(Italian Rates, English Rates, American Rates, Russia rates na Polish
rates), kwa Afrika nzima ukiangalia hatujawahi kuwa na viwango vya
Utalii.
Ingawa
kunaviwango mbalimbali vya kanda lakini kwa sasa ni zamu ya Bara
laAfrika Kupanfa viwango hivyo ili vimwezeshe kila Mwafrika Kutembelea
Vivutio vya Afrika Nzima." Alisema Leina.
Kuna
kanda mbalimbali ambazo zinaambazo zimeweka viwango vyao vya utalii
mfano Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi,
Rwanda na Sudani kusini wazawa wa Afrika Mashariki wananufaika na
viwango hivyo, ukienda nchi za Afrika Magharibi ambazo ni
Benin,
Burkina Faso, Cape Verde, Ivory Cost, Gambia, Ghana, Guinea,
Guinea-Bissau, Liberia, Mali, Niger, Nigeria, Senegal, Sierra Lieoni na
Togo (ECOWAS), Unapata viwango vya utalii vya (ECOWAS Rates) na Ukienda
nchi za Kusini mwa Afrika unakuta (SADC Rates) Viwango hivyo vyote ni
kwa nchi za kanda.
Na
mtu kutoka nchi nyingine ambaye hajui viwango vya bei za utalii akienda
kutalii vivutuo vilivyopo nchi nyingine analipishwa kama mzungu ambaye
anakiwango chake cha utalii.
“Sasa
hii Taasisi yetu ya Intra Africa Traveller Vature fare Initiative lengo
letu ni kuhakikishatunahamasisha watoa huduma za utalii ambao ni
‘Camps’, mashirika ya Ndege na hoteli ziweze kutoa viwango ambavyo
tutaita na sisi ‘African Rates’(Viwango vya fedha za Utalii kwa
Afrika).” Alisema Leina.
Licha
ya hayo watoa huduma za utalii wakishatoa viwango hivyo vya Utalii kwa
kwa nchi za bara la Afrika ambapo zitaunganishwa na Viwango vingine vya
mabara mengine katika utalii wa wazawa wa Afrika.
Leina Amesema kuwa ili kuhakikisha utalii wa wazawa wa Bara la Afrika linakuwa zaidi kama nchi za mabara mengine.
“Soko
la Utalii liweze kugundua kuwa waafrika naowanaweza kusafiri kwenda
kwenye vivutuo vilivyopo barana. Kama nasisi tutakuwa na gharama nafuu
kwaajili ya kutalii katika vivutio vilivyopo barani mwetu.” Amesema
Leina.
Leina
amesema kuwa nchi zaidi ya 12 za bara la Afrika walishiriki katika
Mkutano wa Mtandaoni (Video Conference) na watu zaidi ya 125 walishiriki
kikamilifu kutoa maoni yao juu ya kushirikiana pamoja kupanga Viwango
vya fedha za Utalii za Bara la Afrika.
Alisema
kuwa kila nchi ilionesha kuwa inakivutio gani cha utalii ambacho
kitamwezesha mzawa wa Bara la Afrika kutembelea nchi za Bara hili.
“Waliohudhulia
mkutano huo wengi walisema hawakujua kama Bara la Afrika linavivutio
vizuri kama tulivyoongea leo sasa inatakiwa tuvitembelee.” Alisema
Leina.
Hata
hivyo Leina alisema kuwa waliendelea kuongea na watoa huduma mbalimbali
za utalii katika bara nzima la Afrika kwaajili ya kuangalia ni namna
gani watashirikiana katika kupanga viwango vya mzawa wa bara la Afrika.
Alisema
kuwa kila aliyeshiriki mkutano wa mtandaoni alikubali kuanzisha Viwango
vya Fedha za utalii kwa wazawa wa Bara la Afrika (Afrikani Rates).
Mafanikio
Kwa
hapa nchini kampuni ya kwanza kuanzisha Viwango vya Utalii kwa wazawa
wa Bara la Afrika ni Coastal Aviation na ukiangalia kwenye tovuti vya
Coastal Aviation wao wanaviwango vya fedha za Utalii kwa wazawa wa Bara
la Afrika, hii inamanisha kuwa kwa mwafrika yeyote anayekuja Tanzania
akitaka kutembelea Vivutio vya Tanzania anakutana na Viwango vya utalii
vya Afrika (African Rates).
Ukitembelea
Vivutio vya Afrika ya Kusini wao wanaviwango vya Utalii kwa mzawa wa
Bara la Afrika (African Rates), Kwa Tanzania kunabaadhi ya kampuni kama
Msafiri Travel na baadhi ya hoteli kama Ramada nao wanaviwango vya
Utalii va Kiafrika.
Changamoto
Changamoto
kubwa iliyopo Leina alisema kuwa Waafrika tunashindwa kusafiri katika
Bara la Afrika kutokana na gharama kubwa za huduma za utalii.
Hata
hivyo Leina amewahamasisha wazawa wa Bara la Afrika wote wanaposafiri
kutembelea vivutio vya barani Afrika, kuulizia viwango vya fedha za
utalii(Africa Rates) na wasiogope kuuliza gharama za utalii za
Kiafrika.
0659481912
No comments :
Post a Comment