Spika wa Bunge, Job
Ndugai akifungua warsha ya wabunge kuhusu vitendo vya unyanyasaji wa
watoto wakati wa kuadhimisha Siku ya Watoto Duniani kwenye Ukumbi wa
Msekwa, bungeni jijini Dodoma Novemba 202, 2020. Warsha hiyo iliandaliwa
na Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na Watoto (UNICEF).
Kutoka Kulia ni Katibu wa Bunge, Dk. Steven Kagaigai, Naibu Spika wa
Bunge, Dk. Tulia Ackson na kutoka kulia ni Mwakilishi wa UNICEF, Shalini
Bahuguna na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Zlatan Milisic.
Mariam Mmbaga (26)
ana digrii ya Mawasiliano ya Umma ni mmoja wa vijana waliohusika
kukusanya mawazo ya watoto na vijana Tanzania Bara na Zanzibar kuunda
ahjenda ya watoto na vijana.
Rose Mweleka (24) ni mfamasia mwenye digrii aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Kampala, Dar es Salaam. Anatumia muda wake kuwafundisha viongozi vijana kusaidia kufanya mabadiliko katika jamii.
Baadhi ya wabunge wakisoma nyaraka walizogawiwa na UNICEF
Shemu ya wabunge wakiw makini kusikiliza
Agape Joster (13)
aliyemaliza darasa la 7 katika Shule ya Mushewe mkoani jijini Mbeya,
alikuwa ni Mjumbe wa Klabu ya Tuseme, akielezea jinsi ya kunawa mikono
kujikinga na ugonjwa wa Corona.
Abdulatif Hassan (16), Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Chuini Zanzibar ambaye pia ni mtangazaji wa Kituo cha Radio cha Zenj FM akielezea jinsi watoto wenye virusi vya UKIMWI wanavyo nyanyapaliwa katika jamii.
Baadhi ya maofisa na wabunge
Mwakilishi wa UNICEF, Shalini Bahuguna
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Zlatan Milisic.
Spika Ndugai akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo.
Spika wa Bunge, Job
Nduga (katikati) Katibu wa Bunge, Dk. Steven Kagaigai (kulia) , Naibu
Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson wakiangalia filamu iliyohusisha watoto
na vijana.
Naibu
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akifunga warsha hiyo kwa kusisitiza
kuwatendea haki watoto ikiwa ni sehemu bora ya malezi.
Wabunge wakitoka baada ya warsha kumalizika
Spika wa Bunge, Job Ndugai, Katibu wa Bunge, Dk. Steven Kagaigai (kulia)
, Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson wakiwa katika picha ya pamoja
na watoto, vijana waliokuwaq wasemaji wakuu katika warsha hiyo pamoja na
viongozi wa UNICEF. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
No comments :
Post a Comment