Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Ujumbe
wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Kampuni 13 nchini Austria
umeridhishwa na Uwekezaji nchini Tanzania katika Sekta mbalimbali za
Kilimo, Afya, Miundombinu, Anga, na Ujenzi wa Viwanda.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Dkt. Maduhu Kazi amesema lengo kubwa la Ujumbe huo ni kuangalia vivutio vya Uwekezaji nchini Tanzania, amesema hadi sasa Austria inategemea kuwekeza katika Miradi 11 wakati mazungumzo katika Uwekezaji wa Miradi hiyo unaendelea vizuri.
Dkt. Maduhu amesema si Austria pekee wanaotaka kuwekeza nchini bali kuna nchi nyingi ambazo zimeridhishwa na hali ya Utulivu na Usalama, Hali ya Uwekezaji na Ukuaji mkubwa wa Uchumi (Uchumi wa Kipato cha Kati).
“Kuna fursa nyingi za Uwekezaji kuna Kampuni nyingi zinatuamini, kwa kuwa sasa tumejiwekeza zaidi katika viwanda na masuala ya Teknolojia pia kuongeza thamani kwenye mazao ya Kilimo”, amesema Dkt. Maduhu.
Baadhi ya Wawekezaji hao, Balozi Mkazi wa Austria, Christian Fellner amesema wamefurahi kuwepo nchini Tanzania kwa ukaribisho mzuri wa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, amesema wamekuja nchini na Kampuni ambazo zitasidia katika Usalama wa Anga, masuala ya Elimu, Ulinzi ikiwa kuangalia uwekezaji baina ya nchi mbili za Tanzania na Austria na baadae wote kupata faida katika uwekezaji huo.
Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dkt. John Simbachawene amesema Ujumbe wa Wawekezaji hao umeridhishwa na Uwekezaji nchini, kutokana na kuwepo mazingira safi na mazuri ya Uwekezaji huo ikiwemo Ukarimu wa Watanzania.
Hatua hiyo ya kuukaribisha Ujumbe huo kutoka Austira ni utekelezaji wa wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa kuelekeza zaidi katika kukuza Uchumi Taifa kupitia Sekta Binafsi na Uwekezaji.
No comments :
Post a Comment