Mkurugenzi wa Programu za Jamii-TASAF
Amadeus Kamagenge(aliyesimama) akifungua
kikao kazi cha Wawezesha wa kitaifa wa zoezi la kuhakiki Walengwa waTASAF ,kulia
kwake ni meneja wa Masjali ya walengwa wa TASAF,Bi. Phillipine Mmari na
kushoto ni Mtaalamu wa Mafunzo Bi. Mercy
Mandawa.
Baadhi ya Wawezeshaji wa kitaifa wa zoezi la Uhakiki wa Walengwa wa TASAF,wakiwa
kwenye ukumbi wa ofisi ndogo ya TASAF
jijini Dar es salaam wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi hicho iliyotolewa na Mkurugenzi
wa Programu za Jamii Amadeus Kamagenge (hayupo pichani).
Na Estom Sanga-TASAF
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF umeanza awamu ya pili ya
zoezi la uhakiki wa Walengwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo laRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
alilolitoa wakati wa uzinduzi wa Kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya TASAF
mwanzoni mwa mwaka huu jijini Dar es salaam.
Akifungua
kikao kazi cha Wawezeshaji wa kitaifa kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi ndogo
ya TASAF jijini Dar es salaam, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa
TASAF,Ladislaus Mwamanga,Mkurugenzi wa Programu za Jamii Amadeus Kamagenge
amesisitiza umuhimu wa kutekelezaji zoezi la uhakiki wa Walengwa kwa umakini
mkubwa ili kuondoa uwezekano wa kuwa na walengwa wasiostahili kunufaika na
huduma za Mpango.
‘’Uhakiki
na uandikishaji sahihi wa Walengwa ndiyo Msingi wa kuwapata Walengwa sahihi wa
kuhudumiwa kwenye Mpango’’ amesisitiza Kamagenge.
Amesema
licha ya mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shughuli za Mpango ,TASAF imeweka
uzito mkubwa kwenye zoezi la uhakiki wa Walengwa ili wanaokidhi vigenzo ndio wanufaike kama
ilivyoagizwa na serikali.
Akitoa
maelezo ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya zoezi la uhakiki wa Walengwa
,Meneja wa masjala ya Walengwa wa TASAF ,Bi.Phillipine Mmari amesema asilimia
80 ya Walengwa walihakikiwa katika awamu hiyo iliyofanyika kote nchini. Na
asilimia 20 watahakikiwa katika zoezi litakalofanyika katika awamu ya pili.
Serikali kupitia TASAF inatekeleza kipindi cha Pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini ambacho kinatarajiwa kuhudumia takribani Kaya milioni
MOJA na Laki NNE ili kuwawezesha wananchi wanaoishi katika umaskini uliokithiri
kupata fursa ya kukuza kipato na kuboresha
miundombinu katika sekta za elimu,afya na maji.
No comments :
Post a Comment