Kituo kipya Cha
Mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi Cha Mbezi Luis kimeanza rasmi
majaribio leo ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar
Kunenge amesema kwa Sasa kituo hicho kinaweza kuanza kutumika Kutokana
na miundombinu muhimu ya kituo kuwa Katika Hali mzuri.
Akizungumza wakati wa
zoezi la majaribio lililowahusisha Askari wa usalama barabarani na
Wadau wa vyombo vya usafiri, RC Kunenge ameshuhudia Mabasi yakiingia na
kutoka pasipo usumbufu wowote.
Aidha RC Kunenge
amesema kwa Sasa kinachoendelea ni matengenezo madogomadogo ya
umaliziaji wa jengo na miundombinu mingine ambapo Hadi Sasa Ujenzi
umefikia zaidi ya 90%.
Pamoja na hayo RC
Kunenge amesema Ujenzi wa barabara ya kuingia kituoni hapo nao
unaendelea vizuri chini ya Wakala wa TANROAD ambapo amewahimiza kuongeza
kasi ili wakamilishe mradi mapema.
Hata hivyo RC Kunenge
ameongeza kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha maagizo ya Rais Dkt. John
Magufuli ya kutaka Ujenzi ukamilike mwishoni mwa mwezi huu yanatimia.
No comments :
Post a Comment