Katibu tawala mkoa wa
Arusha Richard Kwitega akiongea na wanahabari mara baada ya kufungua
mkutano wa Kamati za Maafa kwa mikoa miwili ya Kilimanjaro na Arusha
ulifanyika jijini Arusha.picha na ahmad Mahmoud
Washiriki wa Mafunzo
ya siku tatu ya kamati za maafa kutoka mikoa ya Kilimanjaro na Arusha
wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa kwenye mafunzo hayo mada
zilizoandaliwa na Ofisi ya Waziri mkuu kitengo cha maafa jijini Arusha
……………………………………………………………………..
Na Ahmed Mahmoud,Arusha
Serikali imetoa Wito
kwa Kamati za maafa za Mikoa kuhakikisha kwamba zinakuwa na mipango
kabla ya maafa na sio baada ya kutokea kwa maafa
Hayo yameelezwa jana
na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Idd Hassan Kimanta katika hotuba yake
iliyosomwa na Katibu Tawala wa Mkoa huo (RAS) Richard Kwitega wakati
wa ufunguzi wa mafunzoya Siku tatu ya Kamati za Maafa za Mikoa ya
Arusha na Kilimanjaro yanayofanyika katika hoteli ya Four Points By
Sheraton Jijini Arusha
Kimanta alisema
majanga ya Ukame,Mafuriko na dhoruba, ajali za barabarani na majanga ya
moto ni baadhi ya maafa yanayochangia idadi kubwa ya vifo vya watu,
magonjwa, ulemavu, na upotevu wa mali
Utafiti unaonyesha
kuwa mvua , vimbuka husababisha robo tatu ya vifo vinavyotokana na
maafa katika mataifa mbalimbali duniani na pia maafa haya yanaathiri
kwa kiwango kikubwa hali ya uchumi
Hivyo alisisitiza
umuhimu wa kuwepo na mipango kwa ajili ya awali kuzuia ama kupunguza
kabla ya kutokea kwa maafa kama hayo kwa kujenga uwezo wa kupunguza
kuanzia ngazi za Vijiji, Wilaya na Mikoa kwa kujiandaa kuwa na wataalam
ili waweze kupatiwa mafunzo, vifaa vya kisasa kwa ajili ya Uokoaji
Mkuu huyo wa Mkoa amesema matukio ya maafa ya asili yanatokana na mabadiliko ya tabiaya nchi katika mataifa mbalimbali duniani
Mafunzo hayo
yamelenga kuzijengea uwezo Kamati za Menejimenti ya maafa ya Mikoa
ya Arusha na Kilimanjaro na Wadau mbalimbali katika masuala ya
menejimenti ya maafa katika Mikoa hii
Mafunzo haya
yameandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu wa Maafa yatawapa
fursa washiriki hao kujadili na kujifunza masuala mbalimbali ya
menejimenti ya maafa juu ya namna ya kuyazuia, kujiandaa na namna ya
kukabiliana na maafa pindi yanapotokea
Pia Washiriki
wataweza kufahamu Sera ya Taifa ya Menejimenti ya Maafa, Mwongozo wa
Taif awa Kukabiliana na Maafa,Sheria ya Mipango Miji na pia Watajadili
Mfumo wa Uratibu wa Maafa hapa nchini Tanzania
Pia watajifunza
Mikakati ya Kitaifa na Kimataifa ili kupunguza athari na pia namna ya
kujiandaa katika kukabiliana na maafa ,upatikanaji na utoaji wa Habari
na mawasiliano wakati wa dharura za maafa, Uratibu wa Maafa katika eneo
la tukio na namna ya utoaji wa huduma ya kwanza kwa Jamii mara maafa
yanapotokea
Serikali imesema
matukio ya maafa ya asili hapa Tanzania yanayotokana na mabadiliko ya
tabianchi yamekuwa yakiongezeka mara kwa mara ambapo Mikoa ya Arusha na
Kilimanjaro ni kati ya Mikoa ambayo imekuwa ikiathirika kwa kiasi
kikubwa.
Mkuu huyo wa Mkoa
ameyataja maafa hayo kuwa ni Ukame , Mafuriko, Magonjwa ya mlipuko
(Kipindupindu) Upepo Mkali, Matetemeko ya Ardhi na Ajali za barabarani
kutokana na Vyombo vya Usafiri
Amesema maafa haya
Pamoja na kuathiri Maisha ya watu pia yamekuwa yakileta madhara
makubwa za Kiuchumi,Kijamii na Kimazingira katika maeneo mbalimbali ya
nchi na kwa kiasi kikubwa huathiri hali ya ukuaji wa uchumi wa nchi
Kimanta aidha amesisitiza kwamba maafa yanapotokea husababisha hasara na madhara makubwa kwa Jamii,Kimazingira na Kiuchumi
Ameeleza kuwa
madhara hayo ni Pamoja na watu kupoteza Maisha, uharibifu wa mazingira,
uharibifu wa miundo mbinu, upotevu wa mali, watu kupata vilema vya
kudumu na Sekta nyingine za Kiuchumi huharibika
Kimanta alisisitiza
kwamba ili kukabiliana na maafa ya aina mbalimbali ili kuokoa Maisha
ya watu, upotevu wa mali, uharibifu wa Miundo mbinmu, Maizingira na
Uchumi nafasi ya masuala ya Utaalam katika kukabiliana na hali hii una
nafasi yake
Alitaja baadhi ya
mikakati hiyo kuwa ni kuimarisha masuala ya Utawala Bora unaotoa nafasi
kw aJamii kushiriki katika kuzuia , kujiandaa na kukabili Maafa ya aina
mbalimbali
Pia kuimarisha elimu
na taarifa kwa wakati katika maeneo mbalimbali hivyo Kamati za Maafa za
Miko ana Wilaya zinawajibu Mkubwa kluhakikisha Sheria, Taratibu,Kanuni
na Miongozo ilkiyopo katika Kukabiliana na maafa inasimamiwa Kikamilifu
ngazi zote
Alitaja Mikakati
mingine katika kukabiliana na Maafa ni suala zima la kuhifadhi mazingira
,Misitu ya Asili.Shiroba za Mapito ya Wanyamapori na Vyanzo vyote vya
Maji
Alisisitiza suala la
kuimarisha utoaji wa elimu ya maafa katika Jamii Vijijini ili Wananchi
waelewe masuala yote ya Menejimenti ya Maafa, Madhara ya Maafa, hatua
Madhubuti za kuchukua ili kupunguza athari za Maafa katika Vijiji vyao
Mkuu huyo wa Mkoa wa
Arusha ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu,Idara ya Uratibu wa Maafa na
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa
Kuandaa Mafunzo haya muhimu kuhusu Menejimenti ya Maafa kwa Kamati hizo
za Maafa za Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro
Mafunzo haya
yanahudhuriwa na Makatibu Tawala wa Mikoa hiyo ya Arusha na
Kilimanjaro,Mwakilishi kutoka UNESCO,Makatibu Tawala Wasadizi wa Mikoa
hii,Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya,Mwakilishi kutoka Wizara ya Habari
,Utamaduni na Michezo, na Wawakilishi kutoka Madhehebu ya Dini kutoka
Mikoa hii
Washiriki wengine ni
kutoka Jeshi la Polisi na Zimamoto kutoka Mikoa ya Arusha na
Kilimanjaro,Waratibu wa Maafa katika Mikoa hii ambapo maada zaidi ya 15
zinawasilishwa na kujadiliwa na washiriki wa mafunzo haya muhimu katika
kukabiliana na maafa katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro
No comments :
Post a Comment