Friday, November 13, 2020

NITAENDELEA KUWAAMINI WANAWAKE KWA KUWAPA NAFASI-RAIS MAGUFULI

Rais wa Jamhuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt.John Magufuli akilihutubia bunge katika Mkutano wa kwanza wa Bunge la 12 bungeni jijini Dodoma

……………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli amesema kuwa ataendelea kuwaamini wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi wake.

Rais Dkt.Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 13 Novemba 2020 bungeni jijini Dodoma wakati akihutubia Mkutano wa kwanza wa bunge la 12.

”Nipende kuwambia wanawake Serikali yangu itaendelea kuwaamini na kuwapa nafasi mbalimbali za Uongozi maana nimeona mnavyochapa kazi ndio maana hata Makamu wa Rais ni Mwanamke”amesema Rais Magufuli.

Aidha Dkt.Magufuli amesema kuwa Serikali yake itaendeleza ushirikiano na Serikali ya Zanzibar chini ya Rais Dkt.Hussein Mwinyi.

“Nipende kumwaahidi Rais Dkt Hussein Mwinyi kuwa kwenye miaka mitano ijayo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatoa ushirikiano mkubwa wa kufanya kazi kwa ukaribu na Serikali ya Zanzibar tutafanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kuleta Maendeleo kwa pande zote mbili za Muungano”amesema Rais Dkt.Magufuli

 

No comments :

Post a Comment