Naibu Gavana wa Benki kuu Tanzania (BOT) Dr.Yamungu Kayandabila akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Wakulima Tanganyika (TFA).
Wanachama wa TFA wakifuatilia kwa makini mkutano
Na John Walter ,Arusha.
**************************************
Naibu Gavana wa Benki kuu
Tanzania (BOT) Dr.Yamungu Kayandabila amekipongeza Chama cha Wakulima
Tanganyika (TFA) kwa kusambaza pembejeo bora kwa Wakulima hivyo kuongeza
uzalishaji na kusaidia upatikanaji wa malighafi katika viwanda .
Akifungua Mkutano Mkuu wa Chama
cha Wakulima Tanganyika (TFA), Naibu Gavana amekitaka chama hicho
kuendelea kushirikiana na taasisi za fedha katika kukuza kilimo ili
kuinua pato la mkulima na taifa kwa ujumla.
Dr.Yamungu amesema kuwa katika
safari ya uchumi wa viwanda wakulima ni wadau muhimu ambao wanapaswa
kuhakikisha kuwa wanazalisha malighafi kwa wingi.
Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa TFA, Peter Sirikwa amesema kuwa walianza kusambaza
pembejeo kwa wanachama wao na wanampango wa kuwafikia wanachama 5,000 na
wakulima walioko nje ya chama hicho.
“Tunaomba serikali itusaidia
kuweka mazingira mazuri ya uagizaji wa pembejeo kutoka nje ili wakulima
wetu wapate pembejeo bora na kwa gharama nafuu” alisema Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi Peter Sirikwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa TFA,
Jastin Shirima amesema kuwa mpango wao ni kuwafikia wakulima wengi na
kusambaza pembejeo ambapo kwa sasa wana vituo 17 nchini vya kusambaza
pembejeo.
Kwa upande Wake Mkulima
aliyehudhuria Mkutano huo Anselim Antony ameipongeza TFA kwa mpango huo
kwani utawawezesha wakulima kuondokana na pembejeo feki.
No comments :
Post a Comment