……………………………………………………………………
NA DENIS MLOWE IRINGA,
MBUNGE wa Jimbo la
Makete ,Festo Sanga, ameahidi kuwasomesha watoto 10 kila mwaka elimu ya
ufundi ikiwa lengo la kuwapata watalaam mbalimbali watakaosaidia wilaya
ya Makete.
Akizungumza wakati wa
Mahafali ya Sita (6) ya Chuo cha Ufundi VETA-Makete, Festo Sanga akiwa
mgeni rasmi alisema kuwa inasikitisha kuona kati ya wanafunzi 64
wanaohitimu chuoni hapo wengi wao ni wanafunzi kutoka nje ya Makete
Hivyo kutokana na
hilo alisema kuwa wanafunzi wanaotokea hapa Makete hawafiki 10, zaidi ya
50 wanatoka nje ya Makete (Mara, Tukuyu, Tanga, Dar es Salaaam, Iringa
n.). Tafsiri yake ni kushindwa kuitumia fursa hii sisi wanamakete hivyo
nitawasomesha wanafunzi kila mwaka.
Sanga ambaye ni mdau
mkubwa wa michezo nchini alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka
vijana wao chuoni hapo waweze kusoma masomo ya ufundi
Amesema kuwa
Serikali imewekeza mabilioni ya fedha katika chuo hiki pekee cha VETA
mkoa wa Njombe, mitambo iliyopo hapa huipati mahali pengine kirahisi
hivyo vijana wajitokeze kwa wingi katika kupata elimu ambayo itasaidia
maendeleo ya Makete na mkoa wa Njombe kwa ujumla.
“Kwa kuanza, mimi
kama Mbunge nitakuwa nasomesha wanafunzi 10 kila mwaka kutoka maeneo
mbalimbali ya kata zetu ndani ya Makete ambao wanauhitaji na
wanamazingira Magumu ya kiuchumi”Amesema
Ameongeza kuwa
kwenye mikutano yote nitaizungumzia VETA MAKETE, kwenye vyombo vya
Habari nitaizungumzia na bahati nzuri ada zake ni nafuu na watanzania
wengi wanazimudu.
Hata hivyo amesema
kuwa hii ni moja ya fursa ya kupata ujuzi wa mambo mbalimbali kama vile
utengenezaji wa batiki, Sabuni, ujenzi wa nyumba, ufundi selemala
ufundi magari, umeme majumbani hivyo vijana watumie vyema uwepo wa chuo
hichi.
“nimeona BATIKI,SABUNI, Ujenzi wa Nyumba, ufundi selemala, Ufundi magari n.k vitu ambavyo ni fursa kwa vijana wa sasa” Alisema
Mhe.Sanga amesema
kuwa anatambua kuna uhaba wa kozi mbali mbali ambazo ni muhimu kama
ufundi bomba, ufundi umeme wa magari,ufundi umeme wa majumba hivyo
kulichukua na kulifanyia kazi.
Wakati huo huo Mbunge
Festo Sanga amekabidhi gari kwa wananchi wa Jimbo la Makete kwa ajili
ya matumizi mbalimbali ambayo ni msiba,dharula n.k,kuzungukia miradi na
utekelezaji wa Ilani kijiji kwa kijiji).
No comments :
Post a Comment