Wednesday, November 11, 2020

MBUNGE ARUSHA MJINI MRISHO GAMBO AAHIDI KUCHAPISHA VITABU 100 VYA KIROHO VITAKAVYOSAMBAZWA NCHI NZIMA


Mbunge Mteule wa jimbo la Arusha Mjini ,Mrisho Mashaka Gambo katikati akizindua rasmi kitabu cha NDOTO NI SHULE YA KIROHO kilichoandikwa na mwandishi wa kitabu Pascal Thomas Makenda aliyeko kulia,uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa huduma ya maombezi wa Radio Safina jijini Arusha

Mbunge Mteule Mrisho Gambo pamoja na mwandishi wa kitambu cha NDOTO NI SHULE YA KIROHO,Pascal Thomas Makenda walionyesha umati wa watu kitabu hicho mara baada ya kuzinduliwa.

Askofu wa kanisa la Bethel World Wide Pantaleo Shao la jijini Arusha aliweka wakfu vitabu hivyo kabla ya kuzinduliwa rasmi na mbunge mteule wa jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo.Na Jusline Marco-Arusha

Mbunge mteule wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Mashaka Gambo ameahidi kuchapisha vitabu 100 vya Ndoto ni Shule ya Kiroho vitakavyosambazwa kwa watanzania nchi nzima.
Gambo ametoa kauli hiyo wakati akizindua kitabu Cha Ndoto ni Shule ya Kiroho,uzinduzi uliofanyika jijini Arusha ambapo amesema kuwa maisha hayahitaji kikata tamaa maana Mungu yupo hai na akitaka makusudio yake yatimie anajua namna ya kuyatimiliza kwa wakati wake.

"Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa ndoto siyo ile ambayo unaiota ukiwa usingizini ndoto ni ile inayokunyima usingizi na ili ndoto iweze kutimia unapaswa kuiweka kwenye matendo."alisisitiza Gambo

Aidha ameongeza kuwa kwenye nyumba ya ibada ndiko mahali salama pa mtu yeyote kukimbilia ambapo ameahidi kushirikiana na huduma ya radio safina ili kuweza kupeleka fursa za kiuchumi kwa kuwapeleka wataalamu wa mikopo kutoa elimu.

"Nitajitahidi kuleta wataalamu wa masuala ya mikopo kuja kutoa elimu ya mambo ya mikopo mahali hapa kusudi fursa za kiuchimi zitakapotokea kipaumbele cha kwanza iwe ni mahali hapa maana naamini mahali hapa ni mahali salama zaidi kwani matarajio yangu nikuona wananchi wa mkoa wa Arusha hususani wanawake wsjasiriamali."alisema Mbunge huyo mteule

Awali akiweka wakfu vitabu hivyo Askofu wa kanisa la Bethel World Wide Pantaleo Shao alisema kuwa kitabu hicho kitamsaidia kila mmoja kuifahamu ndoto yake itakayomuwezesha kwenda mbali kimaisha,kimaendeleo na hata kiuchumi.

Kwa upande wake mwandishi wa kitabu hicho ambaye pia ni mtumishi wa neno la Mungu,Pascal Thomas Makenda alisema kuwa lengo la kitabu hicho ni watu kuweza kufunguliwa,kukutana na nguvu za Mungu,wajifunze namna ya kufunguliwa pamoja na kujifunza namna ya kutoka katika mapito wanayoyapitia.

Ameongeza kuwa kupitia kitabu hicho ni matarajio yake kizazi cha sasa kuweze kumjua Mungu wa kweli wa pekee ambapo amewataka watu kupenda kujisomea vitabu mbalimbali ili kuweza kuongeza uelewa wao.

"Kusoma vitabu inasaidia kufahamu majira ya mtu kutoka katika mateso na mapito hivyo ndani ya kitabu utakana na namna ya kuomba juu ya kibali chako kilichokamatwa,hatma yako ndoto yako malengo yako sambamba na ya kuweza kushinda katika nyakati za raha na ngumu."alisisitiza Pascal Makenda

Vilevile uwekaji wakfu kitabu cha pili cha mtumishi wa Mungu Pascal Thomas Makenda cha Ndoto ni Shule ya Kiroho kimebeba maudhui ya kuwafunua macho watu ili wajifunze neno la Mungu na kujua namna ya kuomba kwa kufunga.


 

No comments :

Post a Comment