Mgeni Rasmi mkuu wa mkoa wa
Geita Mhandisi Robert Gabriel, akizungumza kwenye maonyesho ya Biashara
na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga.
Eneo la maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga, lililopo eneo la Butulwa Kata ya Old -Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akisoma taarifa kwenye maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, akisoma taarifa ya maonyesho hayo ya Biashara na Teknolojia ya Madini.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga
mjini Patrobas Katambi, akizungumza kwenye maonyesho hayo ya Biashara na
Teknolojia ya Madini mkoani Shinyanga.
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, (wa tatu kutoka kulia) akizindua maonyesho ya Biashara na Tekno
lojia ya madini mkoani Shinyanga, wapili kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wa kwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi.
Mkuu wa mkoa wa Geita Robert Gabriel, kulia, akiwa kwenye Banda la Tume ya Madini, akiwa ameshika madini ya Almasi.
Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.
Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.
Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.
Zoezi la ukaguzi wa mabanda likiendelea kwenye maonyesho hayo ya Biashara ya Teknolojia ya Madini.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.
MKUU wa mkoa wa Geita Mhandisi
Robert Gabriel, amezindua rasmi maonyesho ya biashara na Teknolojia ya
madini mkoani Shinyanga, na kuwataka wawekezaji wa madini kwenda
kuwekeza mkoani humo, ili kuunyanyua mkoa huo kichumi na kukua
kimaendeleo.
Uzinduzi wa maonyesho hayo
umefanyika leo Jumamosi Novemba 28,2020 katika eneo la Butulwa Kata ya
Old Shinyanga manispaa ya Shinyanga, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali
wa madini, akiwemo na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas
Katambi na Elias Kwandikwa wa Ushetu, ambayo yatakoma Desemba Mosi mwaka
huu.
Akizungumza kwenye maonyesho
hayo, mkuu wa mkoa wa Geita, ameupongeza mkoa wa Shinyanga kwa kuanzisha
maonyesho hayo, ambayo yatakuwa ni chachu kubwa ya kukuza uchumi wa
mkoa huo.
“Naupongeza sana mkoa wa
Shinyanga kwa kuanzisha maonyesho haya ya Biashara na Teknolojia ya
madini, ambayo ni muhimu sana katika kutangaza fursa za uwekezaji,
pamoja na wawekezaji wadogo wa madini kujifunza namna ya kutumia
Teknolojia za kisasa za kuchimba madini na kupata mali nyingi,” amesema Gabriel.
“Pia nawaomba wawekezaji
wakubwa wa migodi mkoani Shinyanga, mtoe kipaumbele kwa wazawa katika
ajira za migodini, ikiwamo na kusambaza bidhaa mbalimbali ndani ya
migodi hiyo ili wapate kunufaika na rasilimali za nyumbani na siyo kutoa
ajira kwa watu wanje,”ameongeza.
Katika hatua nyingine ameitaka
migodi hiyo mikubwa kuwekeza miradi mikubwa ya kiuchumi mkoani
Shinyanga, ambayo itaacha alama na kuleta maendeleo ili kuubadilisha
mkoa huo kimaendeleo na kuendana na hadhi ya rasirimali ilizonazo, na
siyo kuwaachia mashimo na umaskini mkubwa.
Naye mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Zainab Telack, amesema wameanzisha maonyesho hayo ya biashara na
Teknolojia ya madini, ili kutoa fursa kwa wawekezaji na wafanyabiashara
kuwekeza mkoani humo kwa sababu ni mkoa ambao una madini mengi.
Amesema katika mauzo ya Almasi
kuanzia Julai 2020 hadi Novemba, wameuza Almasi zaidi ya Shilingi
Bilioni 42.5, hivyo haoni sababu ya mkoa huo kuendelea kuwa maskini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geoffrey Mwangulumbi, amesema wazo
hilo la kuanzisha maonyesho hayo lilianza mwaka 2017 hadi 2019, mara
baada ya kufanya utafiti, na kuona Shinyanga imedumaa kimaendeleo kwa
sababu ya kukosekana kwa mzunguko wa kifedha
Aidha amesema maonyesho hayo ya
Biashara na Teknolojia ya madini yatakuwa yakifanyika kila mwaka mwezi
Julai, ili kuongeza thamani ya mnyororo katika Sekta ya madini na
kuuinua kiuchumi mkoa wa Shinyanga.
No comments :
Post a Comment