Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge,
akiwasilisha mada katika Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya
ushirikiano katika siasa, ulinzi na Usalama unaondelea Mjini Gaborone,
Botswana
Mkutano wa Makatibu wakuu ukiendelea mjini Gaborone.
***********************************
Na Mwandishi wetu, Gaborone
Makatibu Wakuu wa
SADC -TROIKA wamekutana na kujadiliana Mambo mbalimbali yakiwemo masala
ya hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ndani ya SADC mjini Gaborone,
Botswana.
Awali, Mkutano wa
Makatibu Wakuu ulifunguliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa wa Botswana, Bw. Gaeimelwe Goitsemang ambae pia
alikuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo.
Ni mara ya kwanza
kwa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (
SADC) kukutana ana kwa ana tangu ulipotokea ugonjwa wa Homa Kali ya
Mapafu (Covid-19).
Kwa upande wa
Makatibu wakuu waliohudhuria katika Mkutano huo kutoka Tanzania ni
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe.
Mkutano wa
Makatibu Wakuu utafuatiwa na Mkutano wa Dharua wa Baraza la Mawaziri wa
Asasi ya SADC ya Ushirikiano katika Siasa, Ulinzi na Usalama baadae leo
mchana mjini Gaborone.
No comments :
Post a Comment