…………………………………………………
Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI
Akiongea leo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 7
wa Afya – Tanzania Health Summit uliofanyika Jijini Dodoma Dkt Kapologwe
amesema zipo changamoto nyingi katika Sekta ya afya, hivyo ushirikiano
wa pamoja utasaidia kutatua changamoto hizo na kuleta mabadiliko kwa
jamii.
Dkt Kapologwe ameendelea kufafanua kuwa Ofisi ya
Rais-TAMISEMI itahakikisha inayaingiza maelekezo yatakayotolewa kwenye
Mkutano huo katika mipango ya Hospitali za Halmashauri, Mikoa, Hospitali
za Kanda na Taifa ili yaweze kutekelezwa kuanzia ngazi ya msingi.
Aidha ameahidi kuwa katika Mkutano wa waganga
wakuu wa Mikoa na Halmashauri ataingiza changamoto zilizotolewa katika
Mkutano huo kwa kuwa wao ni watendaji wakuu katika ngazi ya Mikoa na
Halmashauri lengo likiwa ni kuboresha huduma za afya kwa jamii.
Wakati huohuo rais wa Kongamano la Afya Tanzania
Health Summit, Dkt. Omary Chillo amesema lengo la kongamano hilo ni
kujadili uchumi wa kati unavyoendana na Nyanja ya Afya nchini.
Dkt. Chilo amesema kuwa washiriki ni tasisi
zisizo za kiserikali ambazo zinatoa mada na kujadili jinsi gani wataweza
kuboresha afya ya jamii kwa wananchi.
Hata hivyo, ameeleza
kuwa katika Mkutano huo watatoa mrejesho wa mikutano mingine iliyowahi
kufanyika na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike katika kuboresha Sekta
ya afya katika kipindi hiki cha uchumi wa kati
No comments :
Post a Comment