RAIS wa Zanzibar na
Mwenyekuti wa Baraza la Mapinduzi Dk Huusein Ali Mwinyi amesema
hatasita kutimiza wajibu wake na kwamba wizara zote kwa lengo la kujua
changamoto, na kuondoka urasimu.
Amesema wakati wa kufanya kazi kwa mazoea, kuoneana muhali au wafanyakazi dhamana na viongozi kuzemebea umepita.
Msimamo huo umetolewa
na Rais Dkt Mwinyi alipotemebelea hospitali kuu ya Mnazi Mmoja na
kwenye eneo la biashara huko kijangwani mkoa wa mjini Magharib.
Dkt Mwinyi amesema atakwenda kila wizara baada ya kutembelea hospital kuu na kujionea changamoto zilizopo.
Amesema kuna upungufu wa dawa,mashuka na vifaa vya maabara ambavyo hufanikisha vipimo vya magonjwa mbalimbali.
Aidha amesema
serikali kuu toka Hazina ya smz kati ya Agost na septemba mwaka huu
wizara ya Afya imepokea jumla ya shilingi bilioni 3.1.
Pia amesema pamoja na
fesha hizo bado kuna changamoto hivuo atachukua hatua stahili baada ya
kuzungumza na viongozi, madaktari, wauguzi na wafanyakazi wa hospjtali
hiyo.
Amesema hatantuhumu bila kuwasikiliza kwa haki na wajibu iwapo wanajituma na iwspo wanalipwa stahili zao kwa wakati .
Alipotoka hosputali
kuu Rais Dk Mwinyo ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya
Dk Jamala Adam Taib na Mkurugenzi Mtendaji wa hospjtali ya Mnazi Mmoja
Dkt Ali Salum Alim
Baadae ametembelea
eneo la biashara huko kijangwani na kuutaka uongozi wa Manispaa na Mkoa
wa Mjini Magharib kuhakikisha wanatafuta eno jingine kwa ujenzi wa soko
Aliwaeleza kabla ya
halijapatikana eneo jingine wafanyabiashra hao waachwe na shighuli zao
hadi watakapopelekwa sehemu mbadala..
No comments :
Post a Comment