Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw. Gerald Kusaya ( kulia) akisaini kitabu cha wageni wakati
alipotembelea kukagua shamba la kahawa na migomba la mkulima Mama
Hellena Mtika wa kijiji cha Kinyariri wilaya ya Butiama leo. Shamba hilo
linatumika kama darasa kwa wakulima kufundishwa kilimo bora cha kahawa
na migomba chini ya usimamizi wa TACRI.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( katikati) akikagua
shamba darasa la alizeti akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Anna
Rose Nyamubi ( kushoto) na kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bi.
Karoline Muthapula leo wakati alipotembelea kukagua kituo maalum cha
Mafunzo Wakulima cha Mama Maria Nyerere kilichopo Butiama. Kituo hicho
kimeanzishwa ili kuwa eneo maalum la taasisi za umma na binafsi kuweka
mashamba darasa ya mfano ya kufundisha kanuni bora za kilimo ikiwemo
teknolojia za uzalishaji mazao. Lengo la mkoa wa Mara ni kuwa na viwanja
hiyvo kutumika kama ilivyo viwanja vya Nane nane.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Bw. Gerald Kusaya akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Mara Bi. Karoline
Muthapula (kushoto) mara baada ya kukagua eneo la ekari 3 zilizotengwa
kwa ajili ya wizara ya kilimo na taasisi zake kuanzisha mashamba darasa
kwenye viwanja vya Mama Maria Nyerere Butiama. Akiwa katika eneo hilo
Kusaya ameagiza Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Mbegu (ASA) Dkt. Sophia
Kashenge kwenda Butiama na kuanzisha shamba darasa la kufundishia
wakulima ubora wa mbegu zinazozalishwa ili kujenga imani ya ubora na pia
kuvutia masoko. Aidha, ameagiza taasisi ya utafiti TARI kwenda haraka
Butiama na kuanzisha shamba darasa la mbegu za mihogo ikiwemo kufundisha
matokeo ya utafiti wa visumbufu vya mihogo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya ( kushoto) akitazama samaki
wanaofugwa kwenye vizimba alipotembelea mradi wa kufuga samaki kwenye
vizimba Rwamkoma JKT katika bwawa la Kyrarano wilaya ya Butiama. Uongozi
wa wilaya ya Butiama umeomba wizara ya Kilimo usaidie kufufua skimu ya
umwagiliaji katika eneo hilo ili wakulima wazalishe mazao kama ambavyo
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikusudia kwa
kujenga bwawa hilo.
( Habari na picha na Wizara ya Kilimo)
**************************************
Serikali
imeupongeza uongozi wa mkoa wa Mara kwa mkakati wake wa kufufua zao la
kahawa sambamba na mazao ya pamba na mkonge ili kuwa na uhakika wa
kipato kwa wakulima wake.
Pongezi
hizo zimetolewa leo ( 20.11.2020) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo
Gerald Kusaya aliyetembelea kituo maalum cha mafunzo ya wakulima kwenye
viwanja vya maonesho vya Mama Maria Nyerere wilayani Butiama .
”
Naupongeza sana uongozi wa mkoa wa Mara kwa jitihada zake za kufufua
mazao ya kimkakati ikiwemo kahawa,pamba na mkonge kwani yana mchango
mkubwa katika kumaliza umasikini wa wananchi wetu” alisema Kusaya.
Akiwa
Butiama Kusaya alipokea taarifa ya wilaya iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya
hiyo Anna Rose Nyamubi aliyesema wamepanga kuongeza uzalishaji wa zao la
kahawa kwa kupanda miche 340,000 ili baada ya miaka mitatu wawe na
uwezo wa kuvuna tani 1000 za kahawa kutokana na hali ya hewa nzuri na
utayari wa wakulima.
Mkuu
huyo wa wilaya ya Butiama aliongeza kusema kupitia kituo cha maonesho ya
kilimo ya Mama Maria Nyerere taasisi za umma na binafsi zimeweka
mashamba darasa maalum kufundisha wakulima namna sahihi ya kuzalisha
mazao ya biashara ikiwemo kahawa, pamba, mkonge ,korosho na mazao ya
chakula na mboga mboga.
Mkakati
wa mkoa wa Mara ifikapo mwaka 2023 waongeze uzalishaji kahawa toka tani
1,800 za sasa hadi kufikia tani 15,000 kupitia uhamasishaji wakulima
kuanzisha na kufufua mashamba .
”
Butiama tulipaswa kuwa juu kwenye mafanikio ya kilimo kutokana na hali
ya hewa nzuri,hivyo tunaomba wizara ya kilimo ishirikane nasi
kuhamasisha upatikanaji wa mbegu bora za mazao na pia kufufua skimu za
umwagiliaji ” alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Akijibu
maombi hayo Katibu Mkuu Kusaya alisema kupitia taasisi za utafiti wa
zao la kahawa (TACRI) taasisi ya utafiti wa kilimo (TARI) na Wakala wa
Mbegu (ASA) atahakikisha wanafika mkoani Mara mapema kutoa elimu
,kuzalisha mbegu na kutoa matokeo ya tafiti za kusaidia mkulima kuinua
tija na uzalishaji wa mazao.
Kusaya
alitembelea wakulima wa vijiji vya Kinyariri na Biatika wilaya ya
Butiama kukagua mashamba ya kahawa na vitalu vya miche na kujionea
uhitaji mkubwa wa miche ambapo ametoa agizo kwa TACRI kuhakiksha
inazalisha kwa wingi miche bora ya kahawa na kuigawa kwa wakulima.
” Ni
vibaya kuona wakulima wanahitaji miche ya kahawa halafu tuanyo taasisi
inashindwa kufikisha huduma hiyo kwa wakulima. Nataka kuona jitihada za
TACRI kuzalisha na kusambaza miche bora ya kahawa kwa wakulima wa Mara
haraka” aliagiza Kusaya.
Katika
hatua nyingine Kusaya ameagiza Wakala wa Mbegu( ASA) kupeleka mbegu
bora za mahindi na mazao mengine mkoani Mara na kuuza za bei ya shilingi
5,500 kwa mfuko wa kilo mbili ili wakulima wapande msimu huu wa mvua.
Katika
kuhakikisha mkoa wa Mara unafanikiwa kufufua mazao ya kimkakati Kusaya
ameagiza wataalam wa mkoa kupanga maeneo maalum ya kuzalisha mazao ya
biashara badala ya ilivyo sasa kulima kila eneo au wilaya hali
inayosababisha ugumu kwa wataalam kuwafika wakulima.
”
Tusiwaache wakulima walime kilimo cha mazoea, tuwashauri kitaalam na
kuweka kanda ili wanufaike na utaalam na kuwa tuwashauri wapime afya ya
udongo kabla ya kulima ili wajue aina ya mazao na mbolea ya kutumia kwa
lengo la kuwa na uhakika wa uzalishaji” alisema Kusaya.
Wizara
ya Kilimo kupitia Kituo cha Utafiti wa kilimo (TARI) Selian cha Arusha
tayari wamekusanya sampili 30,400 za udongo kutoka mikoa 18 ya Tanzania
kwa lengo la kupima afya yake na kutengeneza ramani itakayosaidia
wakulima na wawekezaji kujua tabia za udongo kabla ya kuamua kuanza
uzalishaji wa mazao.
Katibu
Mkuu Kusaya alitaja faida za kujua tabia ya udongo ni kumwezesha
mkulima kuachana na kilimo cha mazaoe badala yake alime kisayansi na
kuweza kupata mavuno mengi na bora hatua itakayosaidia kuwa na uhakika
wa masoko.
No comments :
Post a Comment