Mratibu
wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision, Dk. Frank
Mtimba akimkabidhi Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Joachim Otaru
moja kati ya maboksi 424 yenye taulo za kike zilizotolewa na Shirika la
World Vision kwa ajili ya wanafunzi mkoani Shinyanga.
**
Na Kadama Malunde
Shirika
la World Vision Tanzania limetoa msaada wa Runinga 8,Taulo za kike
maboksi 424 na vifaa vya michezo zikiwemo jezi pea 72 na mipira 72
vyenye thamani ya shilingi milioni 62.8 kwa ajili ya shule 18 za msingi
na sekondari mkoani Shinyanga.
Hafla
fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo imefanyika leo Jumapili Oktoba
18,2020 katika Chuo Cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Mjini Shinyanga
ambapo Mgeni rasmi alikuwa Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Joachim
Otaru.
Makabidhiano
hayo ya vifaa yamekwenda sanjari na tukio la kufunga mafunzo ya siku
tatu kwa wanafunzi viongozi wa shule za msingi na sekondari 18 zilizopo
katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Kishapu na Kahama Mji ambayo
yaliandaliwa na Shirika la World Vision kwa lengo kuwajengea uwezo na
uelewa kuhusu Afya ya Uzazi na Ujinsia na Ukatili wa Kijinsia.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa na kufunga mafunzo hayo, Kaimu Katibu Tawala
Mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru alilishukuru Shirika la World Vision
kupitia mradi wake wa ENRICH kwa kutoa mafunzo na vifaa vya michezo na
vya kujifunzia shuleni.
“Nimeambiwa
mafunzo mliyopewa pamoja vifaa hivi zikiwemo Tv, Jezi,Mipira na taulo
za kike zimegharimu takribani shilingi Milioni 62 na laki 8.
Tunawashukuru sana World Vision kwa kuendelea kushirikiana na serikali
katika kuboresha sekta elimu na kusaidia wanafunzi wetu”,alisema Otaru.
Aidha
alitumia fursa hiyo kuwaomba walimu na wanafunzi wa shule zilizopata
msaada huo wa vifaa vya kujifunzia na michezo kutunza vifaa hivyo na
kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Nendeni
mkatumie Runinga hizi kwa ajili kutoa elimu mbalimbali,lakini pia
Walimu hakikisheni taulo za kike zinawafikia walengwa. Takwimu
zinaonesha wanafunzi wa kike wanapoteza miezi miwili katika masomo yao
wanapokuwa katika siku zao hivyo kupunguza kiwango cha ufaulu. Kutokana
na taulo hizi tulizopatiwa ufaulu utaongezeka”,aliongeza Otaru.
Kwa
upande wake,Mratibu wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la
World Vision kwa Ufadhili wa Serikali ya Canada katika mkoa wa Shinyanga
na Singida, Dk. Frank Mtimba alisema shule za msingi na sekondari
mkoani Shinyanga zilizonufaika na mafunzo na vifaa hivyo ni zile
zilizopo katika eneo la Mradi wa ENRICH katika halmashauri ya wilaya ya
Kishapu, Shinyanga na Kahama Mji.
Dk.
Mtimba alizitaja shule hizo kwa upande wa halmashauri ya wilaya ya
Kishapu kuwa ni shule za msingi Isemelo, Ndoleleji na Kanawa na kwa
upande wa sekondari kuwa ni Bulekela,Mangu na Ukenyenge.
Kwa
upande wa halmashauri ya Shinyanga ni shule za msingi alisema ni
Manyada,Nshinshinulu na Kituli na shule za sekondari ni Usanda, Tinde na
Kituli wakati katika halmashauri ya Kahama Mji ni shule za msingi
Penzi, Mwendakulima na Iyenze na shule za sekondari kuwa ni Bugisha,
Mwendakulima na Bukamba.
“Tumetoa
taulo za kike maboksi 424,mipira 72 ambapo kila shule itapata mipira
minne kwa ajili ya michezo ya mpira wa miguu na pete (miwili kwa
wasichana na wavulana miwili),jezi 72 ambapo kila itapata pea 4 (2 kwa
wavulana na 2 wasichana) na Runinga 8 kwa ajili ya shule za sekondari
zenye umeme”,alieleza Dk. Mtimba.
Naye
Mratibu wa Afya ya Uzazi kwa mama na mzazi mkoa wa Shinyanga, Joyce
Kondoro alisema katika mafunzo ya siku tatu kwa wanafunzi 72 kutoka
shule 18 mkoani Shinyanga wanafunzi wamefundishwa kuhusu afya ya uzazi
na ujinsia kwa vijana.
Alizitaja
mada zingine ni kuhusu magonjwa ya ngono ikiwemo UKIMWI, ukatili wa
kijinsia na namna ya kutoa taarifa kama kuna matukio ya ukatili dhidi ya
watoto.
Nao
wanafunzi walioshiriki katika mafunzo hayo akiwemo Nchambi Elias kutoka
shule ya Sekondari Mangu wilayani Kishapu walilishukuru Shirika la
World Vision kwa kuwapatia mafunzo na vifaa ambavyo vitawasaidia katika
kujifunza shuleni.
Afisa
Jinsia na Utetezi wa Shirika la World Vision kupitia mradi wa ENRICH,
Magreth Mambali alisihi wanafunzi kufanya michezo na kuzingatia masomo
yao ili waweze kutimiza ndoto zao.
Kaimu
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru akizungumza wakati wa
akifunga mafunzo kuhusu afya ya uzazi ya kwa wanafunzi viongozi wa shule
za msingi na sekondari 18 zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga,Kishapu na Kahama Mji ambayo yaliandaliwa na Shirika la World
Vision kwa lengo kuwajengea uwezo na uelewa kuhusu Afya ya Uzazi na
ujinsia na ukatili wa kijinsia. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kaimu
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru akiwaomba wanafunzi na
walimu kutunza vifaa vilivyotolewa na Shirika la World Vision
Mratibu
wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision kwa
Ufadhili wa Serikali ya Canada katika mkoa wa Shinyanga na Singida, Dk.
Frank Mtimba akielezea kuhusu mradi wa ENRICH unaotekelezwa katika
halmashauri tatu za mkoa wa Shinyanga ambazo ni Kishapu, Kahama Mji na
Shinyanga.
Mratibu
wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision kwa
Ufadhili wa Serikali ya Canada katika mkoa wa Shinyanga na Singida, Dk.
Frank Mtimba akiishukuru serikali kwa kuendelea kushirikiana na Shirika
la World Vision.
Afisa
Jinsia na Utetezi wa Shirika la World Vision kupitia mradi wa ENRICH,
Magreth Mambali akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Afya ya Uzazi
na Ujinsia kwa wanafunzi wa shule 18 za msingi na sekondari mkoani
Shinyanga na kuwataka wakayatumie vizuri mafunzo hayo na kutunza vifaa
vilivyotolewa la Shirika la World Vision.
Afisa
Jinsia na Utetezi wa Shirika la World Vision kupitia mradi wa ENRICH,
Magreth Mambali akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Afya ya Uzazi
na Ujinsia kwa wanafunzi wa shule 18 za msingi na sekondari mkoani
Shinyanga na kuwataka wakayatumie vizuri mafunzo hayo na kutunza vifaa
vilivyotolewa la Shirika la World Vision.
Mratibu
wa Afya ya Uzazi kwa mama na mzazi mkoa wa Shinyanga, Joyce Kondoro
akielezea kuhusu mada zilizofundishwa katika mafunzo ya siku tatu kwa
wanafunzi 72 kutoka shule 18 mkoani Shinyanga ambapo wanafunzi
wamefundishwa kuhusu afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana.
Afisa
Jinsia na Utetezi wa Shirika la World Vision kupitia mradi wa ENRICH,
Magreth Mambali (kulia) akimkabidhi Kaimu Katibu Tawala mkoa wa
Shinyanga Joachim Otaru ,jezi za michezo kwa ajili ya wanafunzi mkoani
Shinyanga.
Kaimu
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru (wa tatu kulia)
akimkabidhi Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Bakari Kasinyo jezi za
michezo kwa ajili ya wanafunzi.
Zoezi la makabidhiano ya mipira ya michezo likiendelea.
Mratibu
wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision kwa
Ufadhili wa Serikali ya Canada katika mkoa wa Shinyanga na Singida, Dk.
Frank Mtimba akimkabidhi Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Joachim
Otaru moja kati ya TV 8 zilizotolewa na Shirika la World Vision.
Afisa
Jinsia na Utetezi wa Shirika la World Vision kupitia mradi wa ENRICH,
Magreth Mambali (kulia) akimkabidhi Kaimu Katibu Tawala mkoa wa
Shinyanga Joachim Otaru ,TV kwa ajili ya wanafunzi mkoani Shinyanga.
Mratibu
wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision kwa
Ufadhili wa Serikali ya Canada katika mkoa wa Shinyanga na Singida, Dk.
Frank Mtimba akimkabidhi Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Joachim
Otaru moja kati ya maboksi 424 yenye taulo laini/kike zilizotolewa na
Shirika la World Vision kwa ajili ya wanafunzi.
Kaimu
Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga Joachim Otaru (wa tatu kulia)
akimkabidhi Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Bakari Kasinyo taulo za
kike kwa ajili ya wanafunzi.
Mratibu
wa Mradi wa ENRICH unaotekelezwa na Shirika la World Vision kwa
Ufadhili wa Serikali ya Canada katika mkoa wa Shinyanga na Singida, Dk.
Frank Mtimba akimkabidhi mipira na jezi Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa
Shinyanga Bakari Kasinyo (kushoto).
Wanafunzi wa shule za Msingi wakionesha baadhi ya jezi za michezo zilizotolewa na Shirika la World Vision
Wanafunzi wa shule za Sekondari wakionesha baadhi ya jezi za michezo zilizotolewa na Shirika la World Vision.
Nchambi
Elias kutoka shule ya Sekondari Mangu wilayani Kishapu akilishukuru
Shirika la World Vision kwa kuwapatia mafunzo na vifaa vya michezo, TV
na taulo za kike.
Muonekano
wa maboksi yenye taulo laini 'pedi' na maboksi yenye TV kwa ajili ya
wanafunzi katika shule 18 za halmashauri ya wilaya ya Kishapu,Kahama Mji
na Shinyanga, vifaa ambavyo vimetolewa na Shirika la World Vision.
Muonekano wa mipira na maboksi yenye jezi.
Muonekano wa baadhi ya jezi
Afisa
Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, Tedson Ngwale akizungumza wakati
wa makabidhiano ya vifaa na mafunzo kuhusu afya ya uzazi ya kwa
wanafunzi viongozi wa shule za msingi na sekondari 18 zilizopo katika
halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Kishapu na Kahama Mji ambayo
yaliandaliwa na Shirika la World Vision
Kaimu
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Bakari Kasinyo akizungumza wakati wa
makabidhiano ya vifaa na mafunzo kuhusu afya ya uzazi ya kwa wanafunzi
viongozi wa shule za msingi na sekondari 18 zilizopo katika halmashauri
ya wilaya ya Shinyanga,Kishapu na Kahama Mji ambayo yaliandaliwa na
Shirika la World Vision.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
No comments :
Post a Comment