Muonekano wa
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI) wakiwa ndani ya basi darasa wakifatilia kwa makini
mafunzo ya afua za virusi vya UKIMWI mahali pa kazi yanayotolewa na
taasisi binafsi ya Tanzania Youth Alliance (TAYOA) kwa njia ya basi
darasa leo Jijini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) wakiwa katika
picha ya pamoja baada ya kupatiwa mafunzo ya afua za virusi vya UKIMWI
mahali pa kazi yanayotolewa na taasisi binafsi ya Tanzania Youth
Alliance (TAYOA) kwa njia ya basi darasa leo Jijini Dodoma.
………………………………………………………
Na. Majid Abdulkarim – Dodoma
Mafunzo hayo yamefanyika leo Jijini Dodoma kwa
njia ya basi darasa ambapo mada zilizotolewa katika basi hilo ni
Saratani ya Kizazi, Ukweli kuhusu Virusi vya Ukimwi na magonjwa ya
ngono, Ukatili wa kijinsi na magonjwa yasioambukizwa.
Aidha mmoja wa Watumishi kutoka Idara ya
Serikali za Mitaa, Bw. Brian Samweli amesema kuwa basi darasa
limewasaidia kuwa na uelewa zaidi juu ya umuhimu wa kuwa na utamaduni wa
kupima Afya zao mara kwa mara ili kupata hali ya afya zao kutokana na
wataalam wa afya watakavyo kuwa wamewaelekeza baada ya kupima.
“Tukiwa na utamaduni wa kupima afya zetu katika
hospitali na vituo vyetu vya afya itasaidia kujua hali ya afya zetu
jambo litakalosaidia kuwahi kupata tiba haraka iwapo utagundulika kuwa
na changamoto ya kiafya”, amesema Samweli.
Naye afisa mradi wa timiza malengo Ekinala
Kasobile ameeleza kuwa kwa sasa mradi huu unatekelezwa katika mikoa
miwili ambayo ni Mkoa wa Dodoma na Morogoro.
“Awali mradi huu
ulikuwa unatekelezwa katika halmashauri za Bahi, Kongwa, Kondoa na
Mpwapwa kwa lengo la kuifikia jamii ya ndani ya shule na nje ya shule
ili kuhakikisha vijana wanatimiza ndoto zao katika maisha yao”, ameeleza
Kasobile
No comments :
Post a Comment