Na Dixon Busagaga ,Kilimanjaro
BAADA ya kupitia katika
kipindi kigumu kifedha hatimaye Benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (KCBL) ya
mkoani Kilimanjaro imeingia mkataba wa makubaliano na Benki ya CRDB ya
uwekezaji huku kiasi cha Sh Bil saba kikiwekezwa katika benki hiyo .
Hafla ya makubaliano hayo imefanyika mjini Moshi na kuhudhuriwa
na watendaji wa Benki hizo mbili wakiwemo wenyeviti wa bodi za Wakurugenzi ,Naibu
Gavana wa Benki kuu, Dkt ,Bernad Kibese,mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyoenda
sambamba na zoezi la ukataji wa utepe katika Benki ya KCBL akiwa ni Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji .
Katika hotuba yake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB
Abdulmajid Mussa Nsekela iliyosomwa na Afisa Mkuu wa fedha wa Benki ya CRDB ,Fredrick
Nshekanabo alisema Benki ya CRDB imekua
mstari wa mbele katika kushirikiana na serikali na wadau wa maendeleo katika
utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kimaendeleo iliyolenga kukuza uchumi wa
Mtanzania na nchi kwa ujumla wake.
“Ushiriki wetuu na
utiaji saini mkataba wa uwekezaji kati ya CRDB na Benki ya ushirika ya KCBL ni
udhihirisho wa wazi wa adhma ya benki kukwmua jamii kiuchumi na kujenga sekta
tumanini na tabasamu kwa wadau ,wateja na wana hisa wa benki ya KCBL.” alisema
Nsekela.
“Huu utakuwa mwanzo
mpya kwa KCBL kwa Taifa na Serikali ya awamu ya tano ,leo njozi ya muda mrefu
ya kuwa na benki ya ushirika nchini umetimia.”aliongeza Nsekela .
Alisema benki ya CRDB
kama raia mwema mwenye dhamira njema kwa nchi yake itatumia sehemu ya mtaji
wake kuwekeza KCBL bila kuchukua faida wala gawio kwa kipindi cha miaka 3 ili
kuikwamua ki mtaji ,kuongeza ukwasi na kuismamia menejimenti,na utawala bora.
“Uwekezaji huu
unalenga kuhakikisha benki inajiendesha kwa ufanisi na faida ili kuvutia
uwekezaji mpana wa kimtaji toka wana ushirika na vyama vya akiba na mikopo
,Msaada wa benki ya CRDB pia utahusisha kuboresha rasilimali watu na uendelevu wa
menejimenti pale mda wa uwekezaji utakapokoma.” Alisema Nsekela
“Ni wazi kuwa uimara
wa uchumi wa nchi unategemea kwa kiasi kikubwa uimara wa taasisi za fedha na
hivyo kama Benki kiongozi nchini tunao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa
tunashirikiana kwa karibu na serikali katika kuhakikisha sekta ya fedha inabaki
kuwa imara na salama wakati wote.”aliongeza Nsekela
Nsekela alisema pamoja
na CRDB kwenda kufanya uwekezaji wa kimkakati katika benki ya KCBL ,bado CRDB
inaona kilichofanyika ni zaidi ya uwekezaji kwa kusimama katika nafasi kama
benki kiongozi na kutekeleza jukumu la kulinda uimara na usalama wa sekta ya
fedha nchini .
“Tunaimarisha ushirika
kama nyenzo muhimu ya maendeleo kwa jamii na kufufua huduma za kifedha kwa
vyama vya akiba na mikopo na katika kipindi cha uwekezaji wake ,Benki ya CRDB
itatumia rasilimali watu na fedha ili kuifanyia maboresho ya kimkakati ,kimfumo
na kimenejimenti benki ya KCBL.” Alisema Nsekela
“Tunaboresha dhima na
dira yake kutoka kwa benki ya ushirika katika mkoa wa Kilimanjaro na kuwa benki
ya ushirika Tanzania kwa ajili ya wana ushirika Tanzania.”aliongeza Nsekela.
Mgeni rasmi katika
hafla hiyo ,Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji alisema Benki ya
CRDB inaelewa nguvu iliyopo kwenye mfumo mzima wa ushirika na kuamua kwa
usahihi kabisa kutumia nyenzo ya ushirika kama mkakati wa kuwafikishia
watanzania wa kawaida huduma za kibenki.
“Sasa hivi ukitembelea
katika vyama vya Ushirika utakuta CRDB Wakala wanafanya kazi pale ambayo pia ni
fursa kwa Ushirika “alisema Dkt Kijaji.
“Niwapongeze
Wanakilimanjaro hususani vyama vya Ushirika kwa kuunganisha nguvu na kuanzisha
Benki hii ya ushirika (KCBL),pamoja na misukosuko ambayo benki hii imepitia kwa
kisi Fulani ili saidia kuleta nuru kwa vyama vya ushirika na wanaushirika hasa
ukizingatia benki hii ndio muasisi wa mfumo wa stakabadhi ghalani “aliongeza
Dkt Kijaji.
Mwisho
No comments :
Post a Comment