Wednesday, October 14, 2020

WANAHABARI KUTOKA MIKOA YA MOROGORO, DAR ES SALAAM,TANGA,UNGUJA NA PEMBA WATAMBELEA WANUFAIKA WA TASAF MKOANI TANGA


Waandishi wa Habari kutoka Unguja, Pemba, Morogoro, Dar es Salaam na Tanga wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka TASAF na katibu Tawala Mkoa wa Tanga Judika Omar, mara baada ya kufungulia kwa kikao kazi cha kujenga uelewa kuhusu kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF, kikao hicho kilichofanyika Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Mkurugenzi  Mtendaji wa TASAF  Ladislaus Mwamanga, akizungumza katika kikao kazi cha cha siku mbili cha kuwajengea uelewa waandishi wa habari, kuhusu utekelezaji wa kipindi cha Pili cha awamu ya tatu ya TASAF, kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Tanga.
Waandishi wa habari kutoka Pemba, Unguja, Morogoro na Dar es Salam na Tanga, wakifuatilia mada mbalimbali katika  kikao cha kuwajengea uelewa kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF, kikao hicho kilichofanyika Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka TASAF Zuhura Mdungi, akiwasilisha Madhumuni ya kikao kazi cha kuwajengea uelewa waandishi wa habari kuhusu PSSN II, kikao kilichofanyika Halmashauri ya jiji la Tanga.
Mmoja ya wanufaika wa mapango wa TASAF mkoani Tanga Bi.Fatuma Abdalah   akiwa na mume wake wakiwaonesha waandishi wa habari(hawapo pichani) moja ya mafanikio walioyapata kupitia TASAF,ikiwa ni pamoja na kuweza kununua mbuzi na mawe kwa ajiri ya kuanza ujenzi wa nyumba.

Mnufaika wa TASAF kutoka mkoani Tanga Bi Zubeda Rashidi akizungumza na waandishi wa habari waliofika nyumbani kwake oktoba 13  kwa lengo la kumtembelea na kujua maendeleo yake baada ya kuingizwa kwenye mapango wa TASAF.

Waandishi wa habari wakiwa na uongozi wa TASAF wakizungumza na baadhi ya  wanufaika wa mpango wa TASAF

 Waandishi wa Habari kutoka Morogoro, Dar Es Salaam,Tanga,Pemba na Unguja kwa nyakati tofauti wakiwa katika picha ya pamoja na mmoja na wanufaika wa TASAF mkoani Tanga

No comments :

Post a Comment