Tuesday, October 13, 2020

VYAMA VYA USHIRIKI NCHINI VYATAKIWA KUHAMASISHA WANAWAKE KUFANYA SHUGHULI ZAO KATIKA USHIRIKA ILI KUPATA MASOKO NA MITAJI


Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Charles Malunde akifungua kongamano la wanawake kwenye ushirika wa Akiba na Mikopo lililofanyika jijini Arusha.

Baadhi washiriki wa Kongamano la Wanawake kwenye vyama vya ushirima kutoka vyama vya ushirika kwenye mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Mwanza,Mbeya,Dodoma,Pwani,Njombe,Morogoro,Iringa,Kagera,Singida,Ruvuma,Tanga pamoja na Dar es salaam.Na Jusline Marco;Arusha.

Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania Charles Malunde amevitaka vyama vya ushirika nchini kuhamasisha wanawake kujiunga katika vyama hivyo na kufanya shughuli zao katika ushirika ili kuweza kupata masoko na mitaji.

Akifungua Kongamano la wanawake kwenye ushirika wa Akiba na Mikopo katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Ushirika wa Akiba na Mikopo lililofanyika jijini Arusha ambapo amesema kuwa ushirika nchini umekuwa chachu katika kuhakikisha makundi ya watu wa kipato cha chini na maskini ndani ya jamii wanakuwa na chombo cha kuaminika cha kuwawezesha kufikia malengo yao kiuchumi na kijamii.

Aidha amesema pamoja na sekta ya Ushirika kushamiri katika sekta mbalimbali za kiuchumi na vyama kujiendesha kwa kufuata misingi ya ushirika kimataifa bado kuna changamoto katika masuala ya nafasi ya mwanamke kwenye uongozi wa vyama vya ushirika hivyo kusababisaha uwepo ndogo wa ushiriki wa wanawake katika sekta hiyo ambapo amesema hali hiyo ikiendelea itapelekea kutokuwa na uendelevu katika shughuli za kiushirika kwa miaka ijayo.

"Kukosekana kwa chombo cha kitaifa cha kuwaunganisha wanawake katika sekta ya ushirika kunapelekea kulosrkana kwa uwakilishi katika anga za kimataifa na kukosa fursa za kimaendeleo zinazoelekezwa katika makundi hayo"alisisitiza Naibu mrajisi huyo

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha makundi hayo yanashiriki kikamilifu katika shughuli za ushirika nchini,tume ya maendeleo ya ushirika kwa kushirikiana na wadau wengine itahakikisha uhalasishaji unafanyika ili kuongeza ushirikiwa wanawake katika vyama vya ushirika kuwatengenezea mazingira rafiki ikiwemo chombo cha kitaifa kitakachoratibu na kusimamia masuala ya wanawake kwa kuwa idara au dawati la wanawake kwa kila chama cha ushirika nchini.

Vilevile ameeleza ushiriki mdogo wa wanawake katika vyama vya ushirika nchini kunapelekea kuwepo kwa matatizo ndani ya jamii inayovizjnguka kwa kutokuwa na usawa wa kijinsia katika vyama vya ushirika ambapo amesema changamoto hizo zinaweza kuwa historia iwapo jukwaa la wanawake litasimamia kwa karibu na kuzifuatilia changamoto ambazo zinamweka mwanamke nyuma katika maendeleo.

Aidha Malunde amesema katika sensa ya mwaka 2012 wanawake walikuwa asilimia 51.3 na upande wa nguvu kazi walikuwa asilimia 53.3 na idadi ya wanawake waliokuwa wanajishughulisha na biashara ndogondogo naza kati ni asilimia 54 ambapo pamoja na idadi hiyo,wanawake wanaozigikia huduma za kifedha ni asilimia 60 huku wanaume wakiwa asilimia 70 na kwa wale wanaozifikia huduma zisizo katika sekta rasmi ni asilimia 9 na ambao hawazifikii kabisa huduma hizo ikiwa ni asilikia 30 kwa wanawakr na wanaume ni asilimia 26.

Ameeleza kuwa matarajio ya serikali kuwa na jukwaa hilo la wanawake walio katika SACCOS litakuwa chachu ya maendeleo ya ushirika wa Akiba na Mikopo nchini.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa muungano wa vyama vya ushirika wa Akiba na Mikopo Tanzania Somoe Ismail amesema kuwa Kongamano hilo limelenga kuwajengea uwezo wanawake walio katika vyama vya akiba na mikopo ili kuweza kuleta maendeleo chanya kwenye jamii kwani muamko wa wanawake kujitokeza na kuwania nafasi mbalimbali katika jamii umekuwa hafifu.

Aidha ametoa wito kwa wanawake kujitokeza na kujiunga katika vyama vya ushirika na katika taasisi nyingine za fedha kwani wanawake wanaweza kuwa viongozi katika ngazi mbalimbali ndani ya jamii.

 

No comments :

Post a Comment