Wednesday, October 21, 2020

VIJANA WANANUFAIKA NA KILIMO KULIKO WATU WAZIMA.


Mtafiti wa mradi wa Utafiti wa sera za kilimo Afrika (APRA) Prof.Ntengua Mdoe akifafanua kuhusu kilimo biashara cha mpunga, mifugo na hali maisha ya wakulima wadogo katika bonde la Kilombero katika semina ya waandishi wa habari iliyofanyika Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) Mkoani Morogoro.

*******************************

Watafiti wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA katika Utafiti wao wamebaini kuwa

Vijana hasa wa kiume ndio wanaonufaika zaidi ni Kilimo biashara cha Mpunga kwenye bonde la Kilombero ijapokuwa wanachangamoto ya mitaji na kukosa mashamba binafsi.

Hayo yanebainishwa na Prof. Ntengua Mdoe wakati akiwasilisha mada ya utafiti wake kwa  Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Mradi wa utafiti wa Sera za Kilimo barani afrika APRA  iliyolenga kutoa matokea ya utafiti wao kwa jamii kupitia vyombo vya habari.

Akiwasilisha matokeo ya Utafiti wake uliohusu ushiriki wa vijana kwenye Kilimo biashara cha Mpunga kwenye bonde la Kilombero Prof. Mdoe amesema vijana wenye umri kati ya miaka 15-35 ni ambao ni sawa na asilimia 35.5% ya watu ndio wenye kunufaika zaidi katika bonde hilo ukilinganisha Makundi mengine.

Amefafanua kuwa kwenye utafiti wao huo wamebaini kuwa  sio kweli kwamba vijana hawashiriki kwenye shighuli za kilimo bali wanashiriki vizuri kwenye Kilimo biashara cha Mpunga pamoja na kwenye mnyororo mzima wa thamani wa zao hilo katika maeneo mbalimbali.

Amesema kwenye Utafiti huo umebaini kuwa kipato wanachokioata vijana kwenye nguvu wanayowekeza kwenye Kilimo ni kikubwa kuliko nguvu inayowekezwa na vijana wanaofanya kazi zingine hapa nchini.

“Ukiangalia kwenye Utafiti tumebaini kuwa nyumba nyingi zinazoongozwa na vijana zina uhakika mkubwa wa chakula kuliko kaya ambazo zinaongozwa na wazee na watu Wenye umri Mkubwa na hii ni kutokana na mafanikio makubwa wanayoyapata kutoka kwenye Kilimo” Alisema Prof.Mdoe.

Katika mapendekezo ya ya utafiti huo Utafiti huo umetaka Halmashauri na Serikali za mitaa kutenga Ardhi ya Kilimo kwaajili ya vijana kama ambavyo imeelekezwa kwenye sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999 lakini pia kuwasaidia mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana wa asilimia 4%  kwenye mapato ya Halmashauri.

“Tunashauri pia Halmashauri za Wilaya kwa kushirikiana na wadau wengine wa Kilimo kuwawezesha vijana kupata elimu ya Kilimo Bora kupitia mafunzo ili kuongeza tija zaidi na kuachana na Kilimo cha mazoea” Alisema Prof. Mdoe.

Akitoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali ya Wanahabari hao Mkuu wa Mradi huo wa APRA upande wa Tanzania Prof. Aida Isinika amesema vijana wengi wanapenda Kilimo chenye tija na soko zaidi kama vile Mpunga, Vitunguu, Nyanya na mazao mengine.

“ Vijana hawataki mazao ya muda mrefu maana sio wavumilivu saa wanahitaji matokeo ya muda mfupi ndio maana unaona wengi wanakimbilia mazao hayo ambayo wanatumia muda mfupi kupata fedha” Alibainisha Prof. Isinika.

Prof. Isinika amesema mitaji wanayohitaji vijana ni midogomidogo na sio mikubwa sana hivyo wakiwezeshwa kupata itawasaidia sana katika kufanya shighuli za Kilimo kwa urahisi na kuongeza tija huku wakibiresha maisha yao.

No comments :

Post a Comment