Balozi
wa Tanzania Korea Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka, akimkabidhi
zawadi ya kinyago huku akitoa maelezo mafupi ya maana ya kinyago hicho
Bw. Donghee Choi, katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Seoul.
Mhe.
Balozi Matilda Swilla Masuka akimkabidhi zawadi ya Tingatinga mshindi
wa kwanza wa shindano la “Show Me Tanzania” Bw. Donghee Choi, katika
ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Seoul.
Balozi
wa Tanzania Korea Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka na wafanyakazi wa
Ubalozi wa Tanzania, Seoul wakibalishana mawazo na Bw. Donghee Choi
jinsi ya kuitangaza zaidi “Destination Tanzania”. Bw. Donghee Choi ni
“Travel blogger” maarufu hapa Seoul na amekuwa akisafiri nchi mbalimbali
duniani.
Balozi
wa Tanzania Korea Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka akikabidhi zawadi
ya vikombe vyenye kutangaza utalii wa Tanzania na kahawa kutoka Tanzania
kwa mshindi wa pili wa shindano la “Show Me Tanzania” bwana Suho Lee,
katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Seoul.
Balozi
wa Tanzania Korea Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka akikabidhi “Plaque
of Appreciation” kwa mshindi wa kwanza wa shindano la “Show Me
Tanzania” Bw. Donghee Choi, katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini
Seoul
Mhe.
Balozi Matilda Swilla Masuka akimkabidhi zawadi ya Tingatinga mshindi
wa pili wa shindano la “Show Me Tanzania” Bw. Suho Lee, katika ofisi za
Ubalozi wa Tanzania jijini Seoul.
Mshindi
wa pili wa shindano la “Show Me Tanzania” bwana Suho Lee, akipiga picha
ya vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Tanzania kwa ajili ya
kuzitumia katika mitandao yake ya kijamii. Bw. Suho Lee ni Mwandishi
maarufu wa habari za kitalii hasa utalii wa nchi za kiafrika.
====== ======== ======== ========
“SHOW ME TANZANIA PHOTO CONTEST EVENT”
Katika
juhudi za kuwavutia watalii zaidi kutembelea Tanzania, Ubalozi wa
Tanzania, Korea Kusini ulibuni Shindano la “Show Me Tanzania” ambapo
Wakorea waliowahi kutembelea Tanzania walikuwa wanatuma picha walizopiga
wakiwa katika vivutio vyetu mbalimbali kupitia Akaunti yetu ya
Instagram- tanzaniaembassykorea
Shindano
hilo lililokuwa la siku 10, kuanzia Agosti 31 hadi Septemba 10,
lilikuwa la mafanikio makubwa kwa kuwavutia washiriki 154 ambao
waliposti zaidi ya picha 1100 na kupata likes zaidi ya 37,000. Kwa maana
nyingine katika muda wa siku hizo kumi Ubalozi uliweza kuongeza wafuasi
wapya 300 katika mitandao yetu ya kijamii na kuwafikia zaidi ya watu
37,000 ambao waliziona picha hizo zenye kuonyesha uzuri wa vivutio vyetu
vya utalii, ubora wa huduma za mahoteli, vyakula, na ukarimu wa
Watanzania.
Aidha,
shindano hilo limewachagiza hata wale waliowahi kutembelea Tanzania
kuweka nia ya kurejea tena nchini kwa kuona kwamba kumbe kuna sehemu
nyingine nzuri pia ambazo hawakuweza kutembelea na hivyo kuwapa hamasa
upya ya kutembelea tena Tanzania.
Kwa
upande mwingine picha zilizokuwa zikitumwa zimedhihirisha dhana ya 3600
kwani ziligusa maeneo mbalimbali yakiwemo Mlima Kilimanjaro, Beaches za
Zanzibar, Dar es Salmaam, Bagamoyo, Safari za Mbugani, Spice Tour,
Maeneo ya Kihistoria kama Kilwa, Stone Town nk. Kwa uhakika shindano
lilifana sana na kujidhihirisha Destination Tanzania inajitosheleza.
Kwa
ujumla wake, shindano hilo limeongeza hamasa ya watalii kuja kutembelea
Tanzania, limetuongezea wafuasi wetu katika mitandao ya kijamii,
limefanya baadhi ya makampuni ya utalii kuanza kushirikiana nasi kama
Ubalozi ambapo tumepata timu ya bloggers na influencers ambao tunaweza
kuwatumia tunapotaka kuwafikia watu wengi zaidi kuhamasisha suala zima
la Utalii.
Kupitia
Shindano hili Ubalozi umeendeleza juhudi za kuwavutia wageni hawa kuja
kutembelea Tanzania. Juhudi zingine ni Pamoja na: Ufunguzi wa Blog ya
Kikorea kupitia mtandao wa Naver, ambayo inawafikishia Habari kwa lugha
ya Kikorea; na pia Media FAM Tour iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana
ambapo kampuni 10 (Media, Bloggers and Influencers) walitembelea
Tanzania na kujionea vivutio vya utalii na baada ya kurudi kuandika
Makala kwa muda wa miezi sita.
Makala
hizo zimekuwa chachu na hamasa kubwa kwa umma wa Wakorea. Tunaamini,
kwa kupata Safe Travels Stamp na uwepo wa Standard Operating Procedures
(SOPs), hali ikitengamaa kwenye hizi nchi za wenzetu, tutaanza kupokea
wageni wengi zaidi katika eneo hili la utalii.
No comments :
Post a Comment