Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James(kulia) na Balozi wa Uswisi nchini, Didier Chassot (kushoto) wakisaini mkataba wa msaada uliotolewa na uswisi wenye thamani ya Tsh.Bilioni 39.59 iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James(kulia) na Balozi wa Uswisi nchini, Didier Chassot (kushoto),wakionesha nakala ya mkataba wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa msaada uliotolewa na uswisi wenye thamani ya Tsh.Bilioni 39.59 iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James(kulia) akibadilishana nakala ya mkataba na Balozi wa Uswisi nchini, Didier Chassot (kushoto), wakati wa hafla ya kusain mkataba wa msaada uliotolewa na uswisi wenye thamani ya Tsh.Bilioni 39.59 iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa msaada uliotolewa na uswisi wenye thamani ya Tsh.Bilioni 39.59 iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Uswisi nchini, Didier Chassot akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa msaada uliotolewa na uswisi wenye thamani ya Tsh.Bilioni 39.59 iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, akielezea umuhimu wa msaada wa Faranga za Uswisi milioni 15.75 sawa na Sh. bilioni 39.59 kwa ajili ya Uboreshaji wa Afya na Uimarishaji wa Mfumo wa Afya na Programu ya Kutokomeza Malaria Tanzania kuwa ni pamoja na kuimarisha nguvu kazi inayotumika kuimarisha uchumi wa nchi, baada ya kusainiwa mikataba hiyo, jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot, wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Amina Shaaban na Wajumbe kutoka Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania, baada ya kusainiawa mikataba miwili ya msaada wa Sh. bilioni 39.59 kwa ajili ya kuboresha Sekta ya Afya.
**************************************
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetia saini mikataba miwili ya msaada kati yake na
Serikali ya Uswisi. Katika mikataba hiyo miwili, Serikali ya Uswisi imetoa msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 15.75, sawa na Shilingi za Tanzania Bilioni 39.59 ambapo msaada huo unalenga kusaidia jitihada za Tanzania kufikia malengo ya kusaidia Sekta ya Afya kwa wote na kupunguza malaria nchini.Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mount Meru uliopo katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Doto James ameeleza kuwa, Tanzania imesaini mikataba miwili ambapo mkataba wa kwanza ni msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 9.75, sawa na Shilingi Bilioni 24.51 za kitanzania ambazo zimetolewa ili kugharamia mradi wa uboreshaji wa afya na uimarishaji wa mfumo wa afya (HPSS) na mkataba wa pili ni wa msaada wa Faranga za Uswisi Milioni 6, sawa na fedha za kitanzania Shilingi Bilioni 15.08 zilizotolewa kwa ajili ya kugharamia programu ya kutokomeza malaria nchini Tanzania ambapo kwa mwezi Oktoba 2020 pekee Tanzania imeweza kusaini mikataba ya jumla ya pesa za kitanzania Bilioni 83.69.
“Wakati tunasaini mikataba hii leo, pia ikumbukwe kuwa tarehe 6 Oktoba, 2020 Serikali zetu mbili zilisaini mikataba miwili ya misaada yenye thamani ya Faranga za Uswisi Milioni 17.80, sawa na Shilingi Bilioni 44.10. Kwa hiyo, kwa mwezi Oktoba 2020 pekee tumesaini mikataba ya misaada ya jumla ya Faranga za Uswisi Milioni 33.55 sawa na Shilingi Bilioni 83.69.” Amesema Doto James.
Doto James ameongeza kuwa pesa hizo zitaenda kutumika kuimarisha Mifumo ya Afya hapa Tanzania kwa kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (iCHF) wenye malengo mahususi ya kuimarisha Sekta ya Afya.
Aidha ameongeza kuwa, Faranga za Uswisi Milioni 6 sawa na Shilingi Bilioni 15.08 zilizotolewa kwa ajili ya Programu ya Kutokomeza Malaria Tanzania zitaenda kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na maralia pamoja na kutekeleza mikakati ya kisekta ya kuzuia maambukizi mapya ya Malaria.
“Tutaweka Mpango wa Kudhibiti Malaria Tanzania kwa lengo la kuondoa kabisa vifo vinavyotokana na malaria na kupanua wigo wa maeneo yasiyokuwa na malaria (Malaria Free Zones) hadi nusu ya nchi nzima ifikapo mwaka 2030 kupitia utambuzi wa maeneo hatarishi kwa Malaria nchini” amesema Doto James.
Akizungumza katika hafla hiyo Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot amesema Serikali ya Tanzania na Uswisi wana uhusiano mzuri kwa muda mrefu sasa na wametoa msaada huo ili kuisaidia Tanzania kujiimarisha katika Sekta ya Afya ikiwemo kupambana na kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini Tanzania.
“Mpango mpya wa malaria ambao tumeusaini leo utaenda kumaliza malaria nchini Tanzania kwa faida ya watu wanaoishi hapa” amesema Mhe. Didier Chassot.
Naye mkurugenzi wa kinga Wizara ya Afya Dkt. Leornard Sudi amesema Wizara ya Afya itaenda kutumia fedha hizo vizuri kwa kuimarisha mifumo ya afya na takwimu kwa ujumla ili kuendelea kupunguza vifo vitokanavyo na malaria ambapo mpaka sasa vimepungua kwa zaidi ya asilimia 67.
“Kwa msaada huu ambao tumeupata wa Bilioni 39.59 tutaendeleza kuimarisha mifumo ya takwimu, sisi tunaelewa kwamba takwimu ndio zitaonesha namna gani tunavyozidi kuendelea” amesema Dkt. Sudi.
No comments :
Post a Comment