Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyongo akikata utepe kuzidua kituo hiki Cha mfano kilichopo ITUMBI, Chunya
Naibu Waziri wa Madini akimpogeza Mkurugezi Mkuu wa STAMICO, Dr Venance Mwasse kwa kazi nzuri ya shirika analosimamia
Naibu Waziri akimpogeza Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO,Mej Gen (rtd) Michael Isamuhyo kwa kazi nzuri inayofanywa na STAMICO.
********************************
Shirika ka Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kupaa kwenye sekta ya madini na leo tarehe 21/10/2020 Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)kwa pamoja
wamezidua kiwanda kipya cha mfano cha uchenjuaji kilichopo ITUMBI, Wilaya ya Chunya.Kituo hiki ni muendelozo wa Shirika kuwafikia wachimbaji wadogo ili kuwapatia mafunzo ili waweze kuchimba kitaalamu zaidi. Kituo hiki ni cha tatu kumilikiwa na STAMICO baada ya vituo vya Katente (Bukombe) na Lwamgasa (Geita). Mafunzo yatakayotolewa kwenye vituo hivi ni pamoja na utafutaji, uchimbaji, uchenjuwaji na biashara ya madini kupitia.
Mgeni rasmi wa tukio alikuwa Naibu Waziri wa Madini Mhe. Stanslaus Nyogo.
Mheshimiwa Waziri aliwasisitizia wachimbaji wadogo wa ITUMBI wachangamkie fursa ya kwenda kujifunza kwenye kituo hiki, “Kitumieni kituo hiki ili mjifunze njia za Kisasa za uchimbaji dhahabu ili muondokane na uchimbaji wa kibahatisha” Alisisitiza Mheshimiwa Waziri.
Wageni wengine waliohudhuria ni pamoja na Katibu Mkuu Madini, Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO na Viongozi wengine kutoka Wizarani na mashirika ya Umma na wananchi wa Wilaya ya Chunya.
No comments :
Post a Comment