……………………………………………………………………..
Wakazi wa kata ya Ninga tarafa
ya Lupembe wilayani Njombe wapo mbioni kuanza kunufaika na mradi wa maji
unaojengwa katika kijiji cha Ninga wenye thamani ya zaidi ya mil mia
560
Kuanza kutekelezwa kwa mradi huo
ambao kwa muda mrefu ulikuwa ukisubiliwa kuwasukuma wananchi kuwa na
moyo wa kufanikisha ujenzi kwa wakati kwa kushirikiana na watalaamu
kutoa nguvu kazi na vifaa visivyopatikana madukani ili uweze kukamilika
kwa wakati na kuanza kunufaisha wananchi.
Fredrick Damian Miale mwenyekiti
wa kijiji na Amina Shorongo ni baadhi ya wakazi wa Ninga ambao wanasema
kwa kipindi kirefu akina mama wamekuwa wakitembea umbali mrefu wa zaidi
ya km 2 hadi 3 kufata maji mabondeni hali ambayo inawafanya kupoteza
muda mwingi na kurudishwa nyuma kiuchumi.
Wamesema endapo mradi huo
utakamilika utawafanya kutekeleza kampeni ya nyumba ni choo kwa asilimia
100 na kukabiliana na magonjwa yatokanayo na uchafu kwa kuwa kutakuwa
na maji ya kutosha ambayo ni muhimu katika kupambana na uchafu.
Awali akizungumzia mradi huo
Fundi Sanifu kutoka wakala ya usambazaji maji safi na usafi wa
mazingira vijijini Ruwasa Joakimu Sanga amesema utatekelezwa kwa kutumia
false akaunti ambapo vituo vya maji 29 na mitandao ya maji itajengwa,In
take,Nyumba ya mlinzi na Pampu pamoja na Tenki lenye mita 8 lenye ujazo
wa mita elfu 1000,
Aidha Sanga amesema mafundi
wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wa kijiji hicho kwani
walikuw tayari muda wote kujitokeza kuchimba mitaro,mashimo na kusogeza
vifaa vya ujenzi huo ambacho umekuwa na kiu ya muda mrefu kwa wananchi.
” Kukamilika kwa mradu huu
kutawafanya wakazi wapatao 2756 kijiji cha Ninga kunufaika na huduma
hiyo ambayo muhimu kwa maisha ya binadamu,Alisema Joakim Sanga.
Kwa upande wake mkurugenzi wa
kitengo cha manunuzi kutoka wizara ya maji Dr Christopher Nditi akiwa na
timu ya watalaamu kutoka wizarani ameridhishwa na mwenendo wa
utekelezaji wa miradi mingi ya maji katika mkoa wa Njombe na kudai
serikali imekusudia kumtua ndoo mama kichwani kwa kukamilisha miradi ya
maji katika maeneo ya mijini na vijijini.
Dr Nditi ambaye amekagua miradi
mbalimbali ya maji ukiwemo wa Howard Kibena, Ninga ,Kitole na Matembwe
amesema katika ukaguzi huo wamebaini changamoto kadhaa ikiwemo ya
miundombinu ya maji, Mtandao mdogo wa maji katika mradi wa kibena na
kuahidi kwenda kuzitafutia majibu haraka iwezekanavyo.
Kuhusu utekelezaji wa miradi ya
maji katika miji 24 ya Tanzania mkurugenzi huyo amesema mchakato upo
katika hatua nzuri na Njombe ni miongoni mwa miji iliyofadhiliwa na
serikali ya India kutekeleza mradi wa maji
” Ni kwenye Njombe ni moja na
miji 24 ya Tanzania ambayo imeingizwa kwenye mpango wa ujenzi wa miradi
ya maji itakayotekelezwa kupitia fedha ya India , na pindi itakapoanza
kutekelezwa itachukua muda mrefu kidogo wa kuanzia mwaka mmoja hadi
mitatu,Alisema Dkt Christopher Nditi.
Nae mkurugenzi wa mamlaka ya
maji safi na taka mji wa Njombe mhandisi John Mtyauli akielezea
changamoto ya huduma ya maji katika mji wa Njombe ,anasema licha ya
kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa Howard Kibena lakini bado mji wa
Njombe unakumbwa na adha ya maji kwasababu ya kasi ya ongezeko la watu.
Eng Mtyauli amesema mahitaji ya
maji ya mji wa Njombe ni makubwa ikilinganishwa na idadi ya watu hivyo
wanategemea kuwa endapo mradi mkubwa unaotarajiwa kujengwa katika mto wa
Hagafilo utakamilika utamaliza shida ya maji katika mji huo na kuufanya
mgao kuwa historia.
“Njombe inakasi kubwa ya
Ongezeko la watu kutokana na uchanga wake na fursa zilizopo hivyo
kiwango cha maji kinachozalishwa kinashindwa kukidhi mahitaji ya
watu,Alisema eng John Mtyauli.
Timu hiyo ya watalaamu kutoka
wizara ya maji ikiongozwa na Dr Nditi imetembelea na kukagua mradi wa
Howard Njombe mjini,Ninga,Matwembwe na Kitole Ukarawa iliyopo katika
halmashauri ya wilaya ya Njombe.
No comments :
Post a Comment