RC NCHIMBI: CHANGAMKIENI FURSA KWENYE KOROSHO
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi
(katikati) akiwa na Watafiti Waandamizi na Mtaalamu kutoka Kituo cha Utafiti wa
Kilimo TARI Naliendele, na Bodi ya Korosho ofisini kwake jana, mda mfupi baada
ya kufanya mazungumzo ya namna bora ya kuinua ubora wa zao la korosho ndani ya
mkoa huo.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi akiwa na Mratibu wa zao la Korosho
kitaifa, Dkt Geradina Mzena wakiangalia moja ya aina za mbegu bora za korosho.
Mkulima wa Korosho kutoka Singida, Hassan Tati,
akishiriki mafunzo yanayotolewa na TARI Naliendele kwa Maafisa ugani na
Wakulima ya Kilimo Bora cha Korosho eneo la namna bora ya kuandaa shimo kabla
ya kupanda mkorosho kwenye shamba la mfano eneo la Somoku, Kata ya Mungu Maji
Singida jana.
Afisa Kilimo Manispaa ya Singida, Halima
Kalungwana akishiriki kwa vitendo mafunzo hayo.
Mkulima
Seleman Mohamed wa Kata ya Unyianga akiwa kwenye mafunzo hayo.
Afisa
Kilimo Kata ya Msisi Singida, Alphoncina Muna (aliyevaa kofia) akishiriki
mafunzo hayo.
Mtaalamu wa Agronomia kutoka TARI Naliendele
Kasiga Ngiha, akiendesha mafunzo.
Mtafiti Mwandamizi na Mtaalamu wa Magonjwa ya
Mikorosho kutoka TARI Naliendele, Dkt Wilson Nene akiwaonyesha wakulima na
Maafisa Ugani namna magonjwa na Wadudu waharibifu walivyoshambulia moja ya
mkorosho uliopo eneo hilo na namna bora ya kudhibiti hali hiyo.
Watafiti
kutoka TARI Naliendele wakiangalia moja ya mkorosho ulioathiriwa vibaya na
ugonjwa wa Ubwiriunga kwenye shamba la Somoku-Mungu Maji singida jana, kupitia
mafunzo hayo wakulima na Maafisa Ugani wanaendelea kupewa mafunzo ya namna ya
kudhibiti hali hiyo.
Akinamama
wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Mafunzo
yakiendelea.
Mafunzo
yakiendelea.
Mafunzo
yakiendelea.
Mafunzo
yakiendelea.
………………………………………………………………………….
Godwin Myovela na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi amesema wakulima
mkoani hapa wamedhamiria kuwa kinara kwenye uzalishaji wa zao la Korosho
nchini, kutokana na jiografia yake kuwa rafiki kwa ‘Dhahabu hiyo ya Kijani’
ambayo inatajwa kuwa na utajiri mkubwa, huku mfumo wa soko ukiendelea kuwa
wazi, salama na uhakika.
Aidha, watafiti kutoka TARI Naliendele wamebaini, kwa msimu
ujao wa mavuno korosho ya mikoa ya Kanda ya Kati ikiwemo Singida, Morogoro na
Dodoma italeta ushindani mkubwa wa soko kwa viwango na ubora, kutokana na
wakulima wake kuendelea kuzingatia kanuni bora za kilimo cha zao hilo.
Nchimbi akizungumza na Mratibu wa zao la Korosho kitaifa
kutoka TARI Naliendele, Dkt Geradina Mzena ofisini kwake jana, alisema kwa sasa
mkoa huo umedhamiria kwa dhati kuinua tija na uzalishaji sambamba na kutoa
msukumo wa kipekee wa zao hilo kwa ubora na viwango vinavyokidhi soko.
“Baada ya kubaini korosho pia ni zao letu wana-singida, ni mkombozi,
na litaubadili kabisa mkoa wetu kiuchumi na kuondokana na kadhia yoyote ya
kuturudisha nyuma; hicho ndicho kilichotusukuma kuingia jumla jumla katika
kilimo hiki cha kitajiri na cha kimkakati,” alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Alisema mpaka sasa, mkoa huo unamshukuru sana Rais John
Magufuli, ambaye serikali yake ya Awamu ya Tano ndiyo iliyobeba wazo hilo la
kuwa na stratejia makini za kuifanya korosho kuwa na tija na ufanisi
unaoonekana, wazo ambalo limeendelea kuwaletea wakulima wa zao hilo matokeo
chanya, hususani kwenye vita dhidi ya
umasikini.
Hata hivyo, akizungumzia juu ya mradi wa ‘Kilimo cha Pamoja’
au maarufu ‘Kilimo cha Bega kwa Bega,’ kilichoshika kasi kwenye baadhi ya
maeneo ya mkoa huo, Nchimbi alisema kilimo hicho kimelenga kushirikiana ili
hatimaye wakulima waweze kupata huduma za kiugani na agronomia stahiki za
korosho kwa pamoja, usawa na kwa wakati.
“Nawapongeza sana TARI Naliendele na serikali kwa ujumla kwa
mafunzo ya kilimo bora cha korosho mnayoendelea kuyatoa ndani ya mkoa wa
Singida. Lengo la serikali yoyote ni kuwatumikia wananchi wake…tukiwa kwenye
safari ya kuelekea katika Uchumi wa Viwanda, mikoa yote nchini tunatakiwa
tutembee pamoja kwa kasi inayodhihirika na ya kuaminika, tusibaguane” alisema Nchimbi.
Mkoa huo ambao una nadharia ya “Twende Wote” “Twende
Pamoja” katika kukuza uchumi na kuifanya
Singida kuwa ya Viwanda, kwa sasa umegeuka kuwa kivutio kikubwa cha ustawi wa
zao la korosho, na zaidi unatajwa kuwa miongoni mwa mikoa ya Kanda ya Kati, ambao
unaanza kwenda kuzalisha korosho kwa kasi na yenye tija stahiki.
Nchimbi alisema wakati wa utekelezaji wa nadharia ya ‘Singida
Twende Pamoja kwenye zao la korosho huwa hakuna bingwa, hakuna mzoefu wala mkuu,
ndio maana kuna ufanisi. “Inapofika wakati wa kupanda tunapaswa tupande wote,
tupalilie pamoja, tupulize viuatilifu pamoja, tuokote wote, na pia tuuze wote.”
Kwa upande wake Mratibu wa zao la Korosho Kitaifa, kutoka
Naliendele, Dkt Geradina Mzena alimshukuru na kumpongeza ‘mama’ Nchimbi kwa
kuwa balozi mzuri kwa wana-singida wote, na hasa pale anapobaini fursa amekuwa
mstari mbele kuiboresha na kuipa msukumo wa kipekee kwa maslahi ya mkoa huo.
Mzena akizungumzia aina za mbegu bora 54 za korosho, alisema
mbegu hizo baada ya kufanyiwa utafiti zimethibitika pasipo shaka kuwapo kwa
ongezeko la thamani, ubora na kiwango cha juu cha uzalishaji, sambamba na kuwa
na uwezo mkubwa wa kuhimili magonjwa na wadudu waharibifu, ikilinganishwa na za
kienyeji.
No comments :
Post a Comment