Afisa uhamiaji Mkoa wa Kagera Kamishina msaidizi Hamza Ismail Shaban akiongea na waandishi wa habari mjini Bukoba katika ofisi za idara hiyo kuhusu kukamatwa kwa raia wa Pakstan aliyeengia nchini Kinyemela.
Wa kwanza kulia ni mtuhuiwa Mohammed Adinani Tahir Raia wa Pakstan aliyengia kinyemela nchini Tanzania akitokea nchini Uganda akitoa maelezo yake kwa waandishi wa habari mjini Bukoba baada ya kukamatwa akitaka kupanda ndege.
**************************************
Na Allawi Kaboyo- Bukoba.
Idara ya uhamiaji mkoani Kagera inamshikilia mtu mmoja raia wa Pakstan aliyeingia nchini kinyume na taratibu akitokea nchini Uganda Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutangaza Tanzania ni salama na hakuna Corona.Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari mjini Bukoba October 8,mwaka huu, Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kagera Kamishina msaidizi Hamza Ismail Shaban amesema kuwa katika utaratibu wao wa kila siku wa kuhakikisha watu wanaoingia na kutoka wanakuwa ni Raia au watu wanaostahili kuwemo nchini, oktoba 7, mwaka huu katika uwanja wa ndege uliopo Bukoba afisa aliyekuwa zamu aliweza kumkama raia huyo akitaka kupanda ndege kuelekea jijini Dar es salaam.
Shaban amesema kuwa raia huyo alitambulika kwa jina la Mohammed Adinani Tahir aliyeingia Tanzania upande wa Kagera akitokea nchini Uganda kwa kupita njia zisizo rasmi.
“Mkoa wetu kama tunavyojua unapakana na nchi mbalimbali, na ikumbukwe janga la Corona kwa nchi za Afrika Mashariki lilikuwa bado ni tatizo na nchi nyingi zilikuwa zimefunga mipaka yake na wananchi wake walikuwa LOCKDOWN na bwana huyu amekaa Uganda kwa takribani miezi 6 kuanzia mwezi wa tatu na amethibitisha ameshindwa kuondoka Uganda kwasababu ya LOCKDOWN na kuamua kukimbilia kwetu japo ameingia kinyemela kwa njia ambazo sio rasmi” Amesema Kamishina Shaban.
Ameongeza kuwa baada ya Rais Magufuli kuitangazia dunia kuwa Tanzania hakuna Corona na shughuli zinaendelea kama kawaida na kuongeza kuwa raia huyo alipata taarifa hizo na kuamua kukimbilia Tanzania na baada ya kuingia akagundua kuwa hakuna Corona ambapo ameeleza kuwa uwepo wake hapa nchini sio rasmi kwakuwa ameingia kinyemela na anaishi nchini kinyume cha sheria.
Kamishina Shaban ametumia fursa hiyo kuwataka raia wanaotaka kuingia Tanzania kufata taratibu zilizowekwa na nchi yetu pamoja na kuwataka watanzania wazalendo kuhakikisha wanawabaini watu wanaoingia nchini kinyemela na kuwatolea taarifa mahala popote watakapo waona.
“Nitoe rai kwa watanzania wazalendo kuwa wasiwe sababu ya watu ambao sio watanzania au ambao hawana vibali vya kuwa hapa nchini kuingia na kuwahifadhi badala yake watoe taarifa kwa idara ya uhamiaji au kwa viongozi wa serikali mahali walipo, kama tunavyojua nchi yetu tupo kwenye mchakato wa uchaguzi hivyo hatupaswi kuruhusu watu wasiokuwa raia au tusiowajua kuingia hapa pasipokujua lengo lao.” Amesisitiza Shaban.
Kwaupande wake mtuhumiwa huyo amesema kuwa amekuja Tanzania baada ya kukaa LOCKDOWN nchini Uganda kwa takribani miezi 6 kutokana na janga la Corona na aliposikia Tanzania hakuna Corona alijaribu kutumia njia mbadala za kuweza kumfikisha hapa nchini ambapo ameeleza kuwa alikuja kwa gari ndogo aina ya Tax.
Amesema kuwa amekuwa akija Tanzania mara kwa mara kutokana na biashara zake anazozifanya hapo awali kabla ya nchi nyingi kufunga mipaka yake kutokana na Corona hivyo Tanzania anaijua.
No comments :
Post a Comment