Friday, October 9, 2020

POLYGOT YATOA MAFUNZO KWA WALIMU KUTATUA CHANGAMOTO ZA UELEWA KWA WANAFUNZI MASHULENI


Mkufunzi mkuu kutoka Tasisi ya Polygot, Mariana Msengi, Akiwafundisah walimu walioshiriki mafunzo hayo maalumu kwa ajili yakuwafundisha watoto .
Mgeni Maalum katika mafunzo hayo Anna Michael Akieleza namna Mariana anavyosaidia watoto wenye uelewa mdogo kutokana na utaalamu wake. 

Walimu na wazazi walioshiriki mafunzo hayo wakifatilia mafunzo kutoka kwa mkufunzi mkuu kutoka Tasisi ya Polygot Mariana Msengi

Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja na mkufunzi mkuu kutoka Tasisi ya Polygot Mariana Msengi

 


Na Mwandishi
Wetu

Walimu na
Wazazi jijini Dar es Salaam wamepatiwa

mafunzo ya kutatua changamoto za uelewa
kwa Watoto wadogo ambao wenye mtaizo ya kuelewa haraka na kisembe pindi
wanapokuwa shuleni na nyumbani kutoka Tasisi ya Polygot House of Language ya
jijini Hapa kwa kushirikiana na ubalozi wa Poland.

Akizungumza na
waandishi wa Habari mara baada ya kuhitimisha mafunzo hayo mkufunzi mkuu kutoka
Tasisi ya Polygot Mariana Msengi amesema wameamua kufanya mafunzo hayo kutokana
na changamoto za ufundishaji walizoziona kwa badhi ya walimu hapa nchini hasa
kwa Watoto wadogo.

 

“walimu
wengi wameshindwa kutofautisha kati ya utundu wa mtoto na kutokuelewa hivyo
hali hii imepelekea walimu wengi kuacha Watoto nyuma wakati wa ufundishaji
hivyo hapa tunawapa mbinu mbadala za kuwasaidia Watoto hawa kupata elimu sawa na
wengine kwani wengi wamekuwa wakiachwa nyuma kutokana na mapungufu yao” Amesema
Mariana Msengi.

Kwa upande
wake mgeni mwalikwa katika progrwamu hiyo Anna Michael amesema kuwa anampenda
Marina kwa kuwa anafundisha Watoto wenye uwezo mdogo na baadae wanafika hatua
mpka wanafaulu darasani kuwa saw ana wale ambao walionyesha uwezo mkubwa hapo
awali.

Anasema kuwa
walimu wengi wana uwezo wa kuwafundisha Watoto wenye akili lakini awajui
kufundisha Watoto wenye uwezo mdogo hivyo mariana amejitolea kufundisha walimu
na wazazi mbinu mbdala hili Watoto wote wawe sawa katika kufundishwa darasani.

Anasema kuwa
kwa sasa wamejenga madarasa lakini wanachangamoto ya thamani za ndani hivyo
ubalozo wa Poland kupitia shirika lake la Polish AID Wameaidi kugharamia
thamani zote zitakazowekwa katika madarasa hayo ya kuwafundisha wakufunzi na Watoto.

 

Kwa upande
wake mmoja wa wanufaika wa masomo hayo Salome Muza amesema mafunzo hayo yamewasaidia
sana kwa kupata uelewa mpya pindi watkapokwenda kufundisha mashuelni
walipotoka.

 

No comments :

Post a Comment