Na Issa Mtuwa – Singida
Mgodi mpya wa Singida Gold Mine, uliozinduliwa mkoani Singida, wilayani Ikungi umeagizwa kuzingatia utoaji wa ajira za wafanyakazi mgodi hapo huku kipaumbele kikiwa kwa wananchi wanaozunga mgodi huo.
Hayo, yalisemwa na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katika hafla
ya uzinduzi wa ujenzi wa mgodi huo tarehe 16 Octoba, 2020. Ameongeza
kuwa uwepo wa mgodi huo utakuwa chachu ya maendeleo kwa Wanasingida na
nchi nzima kwa ujumla.
Nyongo alisema, kwenye mgodi huo una fursa nyingi zitakazotolewa kwa
wananchi kushiriki mambo mbalimbnali ndani na nje ya Mgodi alitoa mfano;
biashara, ulinzi, ajira rasmi na ajira zisizo rasmi. Aliongeza kuwa
kodi itakayolipwa na mgodi kwenye Halmashauri fedha zake zitakwenda
kutumika kwa ajili ya maendeleo Ikungi.
Akizungumzia ulipaji wa maduhuli ya Serikali, Nyongo alisema, Wizara ya
Madini iko mstari wa mbele kuchangia pato la Serikali. Mwaka jana
tulipangiwa kukusanya bilioni 470, mpaka kufikia mwisho wa mwaka, Wizara
iliweza kukusanya kiasi cha bilioni 528. Mwaka huu 2020/2021 Wizara
imepangiwa kukusanya maduhuli ya Serikali bilioni 526.9
Mtendaji Mkuu wa Tume ya Madini, Prof. Shukran Manya, aliemuwakilisha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, alisema kuzinduliwa kwa mgodi huo,
kunaongeza wigo wa kukusanya maduhuli ya Serikali ambayo yanakusanywa na
Tume ya Madini. Hivyo kuwe na mpango waharaka wa kuanza kuzalisha.
Meneja Mkuu wa Singida Gold Mine, Filbert Rweymamu, alimwambia Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Madini, kuwa mgodi umejipanga kushirikiana na
Wanaikungi na kuweka mipango ya kuwainua wananchi kimaendeleo. Alisema
wamepanga kutoa ajira kwa wafanyakazi 200 kipaumbele kikiwa wananchi wa
Ikungi na Singida.
Kuhusu kushirikia na wachimbaji wadogo, mgodi umepanga kutoa mafunzo ya
wachimbaji wadogo kuhusu namna ya uchimbaji salama katika maeneo yao.
Akizungumzia mchango kwa taifa, Rweymamu alisema wanazingatia sheria
mpya ya madini inayoipa Serikali kwa niaba ya wananchi, umiliki wa
asilimia kumi na sita (16% free carried interest) watazilipa kodi kama
zitakavyobainishwa.
Mkuu wa Mkowa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi, alisema amefurahi
kuzinduliwa ujenzi huo ili uanze uzalishaji. Uzalishaji utakapoanza
anategemea vijana wa Singida hawatakuwa na muda kwenda Dodoma Makao
Makuu kwakuwa ajira hapa zitakuwa za kutosha kwa watakao ajiriwa ndani
na wengine watajiajiri kwa kupeleka bidhaa na huduma mgodini.
Kwa Wananchi kwa nyakati tofauti, wamefurahia kuzinduliwa mgodi huo
kwani wanamatumaini kwa kuwa kutakuwa nafursa nyingi zitakazo tolewa.
Wameomba fursa za mgodi wapewe kipaumbele wanaozunguka mgodi.
Waziri wa Madini, Doto Biteko aliwahi kusema; Geita kuna dhahabu lazima
dhahabu iwanufaishe wana Geita, Tanga kuna Vipepeo vya kipekee ambapo
watalii hufika kuviangali, Vipepeo hivyo lazima viwanufaishe Wanatanga,
Shinyanga kuna Almasi, lazima Almasi hiyo iwanufaishe Wanashinyinga,
hata Korosho kule Mtwara lazima ziwanufaishe Wanamtwara. Kwa maelezo ya
Biteko, dhahabu hii ya Singida lazima iwanufaishe watu wa Singida
kutokana na fursa ya uwepo wa dhahabu.
No comments :
Post a Comment