Monday, October 5, 2020

NHIF YAZINDUA MPANGO WA DUNDULIZA KWA HUDUMA ZA BIMA YA AFYA KUPITIA BENKI YA NMB

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)  Bw. Bernald Konga akibadilishana mkataba na Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna mara baada ya kusaini mkataba wa ushirikiano katika uotaji wa huduma ya bima ya afya kupitia huduma ya Dunduliza leo katika ofisi za NHIF mkoa wa Kinondoni jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)  Bw. Bernald Konga akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo leo katikati ni Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna na kulia ni Filbert Mpozni Afisa mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini mkataba huo kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)  Bw. Bernald Konga na kulia ni Filbert Mpozni Afisa mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna katikati na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushoto Bw. Bernald Konga wakisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa huduma ya Dunduliza itakayomfanya mteja kujiwekea fedha na baada ya kutimiza malengo atapatiwa kadi ya bima ya afya kulia anayeshuhudia ni Filbert Mpozni Afisa mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna katikati na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushoto Bw. Bernald Konga wakionesha mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa huduma ya Dunduliza itakayomfanya mteja kujiwekea fedha na baada ya kutimiza malengo atapatiwa kadi ya bima ya afya kulia anayeshuhudia ni Filbert Mpozni Afisa mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB na kushoto ni Christopher Mapunda Mkurugenzi wa Wanachama NHIF.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna katikati na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kushoto Bw. Bernald Konga wakionesha kadi ya Dunduliza baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa huduma ya Dunduliza itakayomfanya mteja kujiwekea fedha na baada ya kutimiza malengo atapatiwa kadi ya bima ya afya kulia ni anayeshuhudia ni Filbert Mpozni Afisa mkuu Wateja Binafsi na Biashara Benki ya NMB.

Picha za pamoja mara baada ya hafla hiyo kumalizika.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na Benki ya NMB wamezindua

mpango unaojulikana kwa jina la DUNDULIZA unaomwezesha mwananchi kudunduliza fedha kidogo kidogo za mchango wa bima ya afya na hatimaye kufanikisha kuchangia kiwango kinachotakiwa na kujiunga na huduma za bima ya afya kupitia NHIF.

Uzinduzi huu umefanyika leo tarehe 05 Oct, 2020 Dar es Salaam ambapo pia uzinduzi huo umeambatana na kusaini makubaliano (MOU) kati ya NHIF na Benki ya NMB ya
namna wateja watakavyoweza kuchangia ama kujiwekea fedha kwa ajili ya kukamilisha mchango wa huduma anazohitaji.

Mpango huu umelenga kuwawezesha wananchi wanaojiunga na NHIF kupitia mpango wa Vifurushi kuweka fedha kidogo kidogo kupitia Benki ya NMB kwa muda
atakaochagua na atakapokamilisha kiwango husika atapatiwa kadi ya matibabu na kuanza kunufaika na huduma za matibabu kupitia NHIF.

Utekelezaji wa Mfumo huu; Mwananchi anayehitaji kujiunga na huduma za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
ambaye atahitaji kuweka fedha kidogo kidogo kwa muda atakaochagua ni yule anajiunga kupitia mpango wa Vifurushi ambavyo vinajulikana kwa majina ya Najali Afya,
Wekeza Afya na Timiza Afya ambavyo pia vinampa fursa mwananchi anayehitaji kuchangia kuchagua huduma kulingana na mahitaji yake, umri na wanufaika anaohitaji
kuwajumuisha.

Mpango huu unamwezesha mwananchi kujiwekea fedha kwa ajili yake mwenyewe, ama kwa ajili yake na mwenza wake ama kwa ajili yake, mwenza na mtoto ama watoto
alionao.
Namna ya kujiwekea fedha kidogo kidogo; Mfumo huu ni rahisi kuutumia kwa kuwa unahitaji mtumiaji kuwa na simu ya mkononi na atazingatia hatua zifuatazo:-
 Utabonyeza *150*68#
 Utachagua namba 2 (Kibubu)
 Utachagua namba 1 (Jisajili)
 Utachagua namba 1 (Kukubali)
 Kisha mfumo utakutaka kuingiza namba ya NIDA na kisha utaendelea na kufuata maelekezo unayopewa kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuanza kujiwekea
fedha kidogo kidogo.

Mfumo huu haubagui mwananchi yoyote kulingana na aina ya simu aliyonayo na endapo atakwama katika hatua za kujisajili anaweza kupiga simu bila malipo kwa namba 0800110063 na utapatiwa maelezo ya namna ya kufanya.

Manufaa ya mpango huu kwa mkulima Kuwepo kwa mfumo huu kunamwondolea mwananchi mzigo wa kulipa fedha zote zinazohitajika kwa mara moja hivyo inampa fursa ya kujipanga na kulipa kidogo kidogo kulingana na muda atakaochagua.

Mfumo huu ambao hauna gharama yoyote kwa mtumiaji unamjengea mwananchi utamaduni wa kujiwekea akiba kupitia Benki na kumwezesha kunufaika na huduma za
matibabu na huduma zingine za kibenki.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa mpango huu, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga alisema kuwa wakati Mfuko unazindua mpango wa Vifurushi Novemba mwaka jana, changamoto iliyoonekana ni pamoja na uwezo wa wananchi kulipa fedha zote kwa awamu moja hatua iliyoifanya Menejimenti ya Mfuko kufungua milango na kuanza kushirikiana na wadau wa taasisi za kifedha kama Benki ya NMB ambayo ina wigo mpana kwa nchi yetu (Ina ofisi kila Wilaya).

“Lengo kubwa la mpango huu ni kumuwezesha mwananchi anayehitaji kunufaika na huduma za matibabu kupitia bima ya afya ili aweze kuweka fedha kidogo kidogo na
hatimaye kupatiwa kadi yake ya matibabu na kuwa na uhakika wa matibabu wakati wote,” alisema Bw. Konga.

Naye Mkurungenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alisema kuwa anafarijika kuzinduliwa kwa mpango huu ambao anaamini utasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kuwa ndani ya mpango wa Bima ya Afya lakini pia kuwajengea wananchi tabia ya kujiwekea akiba kwa matumizi yenye manufaa ya baadae kwao.

“Afya ni kila kitu na hata kwa upande wetu sisi Benki ya NMB tunahitaji sana wateja ambao wana uhakika wa kupata huduma za matibabu wakati wowote na sio wa
kuchukua akiba zao benki kwenda kujitibia, niombe sana wananchi tuutumie huu mpango kuhakikisha wengi wetu tunajiwekea fedha na hatimaye kupata kadi ya
matibabu,” alisema Bi. Zaipuna.

No comments :

Post a Comment