Mhe.
Mohamed Abdallah Mtonga, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja
wa Falme za Kiarabu alifanya mazungumzo na Wakurugenzi wa Kampuni ya Taifa ya
Mafuta ya Abu Dhabi (ADNOC), Bw. Khaled Salmeen, Bw. Iman Al Hosani, Bw.
Mohamed Al Suwaidi na Bw. Abdulla Al Qubaisi kwa njia ya mtandao (Virtual
Meeting).
Balozi
alitumia fursa hiyo kuwajulisha fursa kadhaa zilizopo katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzaia katika eneo hili la Mafuta na Gesi. Maeneo aliyowajulisha
kwa uwekezaji ni yale yaliyohusu uwekaji wa miundombinu katika biashara ya Gesi
na Mafuta. Aidha, Balozi aliwajulisha fursa za kibiashara katika biashara ya
mbolea aina ya Urea kwa utaratibu wa Bulk
Procurement System unaoratibiwa na Tanzania Fertilizers Regulatory
Authority na uletaji wa Mafuta kwa pamoja unaoratibiwa na Bulk Procurement System for Petroleum Products. Bidhaa zote hizi
huzalishwa na Kampuni ya Taifa ya Mafuta ya Abu Dhabi (Abu Dhabi National Oil Company (ADNOC).
Vilevile, Balozi aliwasilisha kwa ADNOC
miradi ambayo ipo tayari kwa uwekezaji iliyopo katika Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (Tanzania Investment Centre) ambayo inatafuta wawekezaji au wabia.
Miradi hiyo ni kama ifuatavyo:
· Establishment of Strategic Petroleum
Reserve Infrastructures (Farm Tanks).
Kwa
mujibu wa andiko Mradi utajikita katika ujenzi wa Matanki ya kuhifadhia mafuta
katika miji ya Dar Es Salaam, Morogoro, Isaka(Kahama),Makambako, Mbeya, Songwe
na Tanga. Watekelezaji wa Mradi huu ni Mwekezaji Mshirika (Strategic Partner)
na Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (Tanzania Petroleum Development
Corporation).
·
LPG
Bulk Distribution Project
Kwa mujibu wa andiko Mradi huu ni
kuweka miundombinu ya Kupokea,kuhifadhi na kuweka miundombinu ya kujaza Gesi
aina ya LPG. Mradi huu utatekelezwa kwa awamu katika miji ya Dar es Salaam, Tanga
na Mtwara. Watekelezaji wa Mradi huu ni Mwekezaji Mshirika (Strategic Partner)
na Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (Tanzania Petroleum Development
Corporation).
Kwa upande wao, Wakurugenzi wa ADNOC wamehitaji taarifa
mbalimbali ambazo Mhe. Balozi Mohamed Mtonga ameziwasilisha katika Kituo cha
Uwekezaji Tanzania kwa kufanyiwa kazi. |
No comments :
Post a Comment