MASHABIKI
wa Hip-hop na wasanii kutoka kote ulimwenguni wameweka REKODI YA DUNIA
YA GUINNESS kupitia video zinazoonyesha wakinachana(rapping)kupitia
mitandao ya kijamii.
Waimbaji
hamsini na moja, waliotamba kwa lugha tofauti tofauti ikiwemo
Kiingereza, Kifaransa, Thai, Urdu, Hindi, Bahasa Indonesia na Kiarabu
walishirikiana kwenye wimbo mmoja ambao ulirushwa moja kwa moja kupitia mtandao.
Baada
ya wengine kulazimika kungojea kwa uvumilivu kwa zaidi ya saa kufikia
zamu yao, watunzi wa nyimbo - pamoja na wadau wa mitandao wenye
followers wengi zaidi waliweza kupaza sauti zao kwa kusheherekea
uzinduzi wa simu mpya ya Infinix Hot 10.
Jitihada za kimataifa, na wafadhili kutoka maeneo mbali kama, Indonesia, Thailand, India, Pakistan, Kenya, Misri na Nigeria
, Walitumia ubunifu huu kama njia ya kuonyesha jinsi vikundi vya watu bado vinaweza kuburudika licha ya kutokuwa pamoja kimwili.
Mwishowe, washiriki 51 walitumia jumla ya saa moja na dakika 11 kuchana (rapping).
Ili kusherehekea rekodi hiyo ya rap, Infinix ametoa video inayoonyesha ustadi wa nyota wa music kutoka nchi mbalimbali.
Video hiyo ikionyesha wakirap ilifungwa na rapa wa Misri Kareem Rafat, na rapa wa China Omar akimaliza wimbo.
Katikati,alipokea
Lerry Khan, nyota wa Tik Tok wa Pakistani mwenye wafuasi milioni moja
Tik Tok pamoja na Tik Tokker Hassan, ambaye ana wafuasi 500,000.
Mmoja
wa waimbaji, Eric kutoka Ufilipino, alisema: "Nilihisi kuheshimiwa na
kufurahi na mafanikio yetu kwa sababu rekodi hiyo haihusiani tu na
shirika moja, lakini sisi sote kama jamii."
Jaribio hilo lilitekelezwa wiki iliyopita na limeridhiwa na REKODI ZA DUNIA ZA GUINESS.
Infinix
ilizindua jaribio la rekodi ya kuonyesha simu yake ya HOT 10, ambayo
ina processor aina Helio G70 yenye ubora kwenye kucheza games, kioo cha
inch 6.78 "HD na betri 5200 mAh.
Msemaji wa Infinix ameongeza: "Infinix Hot 10 ni simu inayoashiria mshikamano na furaha.
Ndio
maana tunajitaidi ili kuvunja GUINNESS WORLD RECORDS kwa kuendelea kuwa
wabunifu na jinsi gani tunaweza kwenda sambamba na teknolojia na
rapping record ya uzinduzi wa Infinix HOT 10.
No comments :
Post a Comment