Naibu
Mkuurugenzi wa Halotel Nguyen Van Trung (Kushoto), Akizungumza na
waandishi wa Habari Makao Makuu ya Halotel katika kuadhimisha miaka
mitano ya utoaji huduma za mawasiliano nchini. Ambapo Halotel wametoa
ofa maalumu ya dabo bando kwa wateja wake ikiwa ni zawadi ya kuadhimisha
miaka mitano (5) Kushoto ni Afisa Mahusiano Stella Pius.
Afisa
Mahusiano Stella Pius akiongea na wandishi wa Habari Makao Makuu ya
Ofisi za Halotel, kuhusiana na ofa maalumu ya wateja wa Halopesa ambapo
mteja atarudishiwa nusu ya makato ya kutuma pesa ikiwa ni zawadi kwa
wateja wao katika kuadhimisha miaka mitano (5) kulia ni Naibu
Mkuurugenzi wa Halotel Nguyen Van Trung.
· Kuongezeka kwa watumiaji wa Halopesa zaidi ya 2.3 Milion
· Wateja kupewa Ofa Maalum
Kampuni
ya Viettel kwa jina la biashara Halotel, siku ya leo inasheherekea
maadhimisho ya miaka mitano ya utoaji huduma za mawasiliano Tanzania,
Kwa muda wote wa utoaji huduma imeweza kufikia malengo kwa viwango vya
juu ikiwemo kuongeza watumiaji wa mtandao huo.
Kutokana
na ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya robo ya pili ya mwaka,
Halotel imefanikiwa kufikisha idadi ya watumiaji wa huduma za
mawasiliano zaidi ya MILIONI 6 mpaka mwezi juni mwaka 2020.
Mafanikio
haya yametokana na ushirikiano mkubwa wa serikali ya Tanzania kwa
kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji, pia watanzania kwa ujumla ambao ni
wateja wetu, wafanyakazi wa Halotel pamoja na ubunifu mkubwa wa kampuni
kwa ujumla kwa kutengeneza huduma zinazokidhi na mahitaji ya
watuamiaji.
Akiongea
na waandishi wa habari Naibu Mkurugenzi wa kampuni hiyo alisema,
“Halotel imekuwa ikitoa huduma ya intaneti kwa shule za msingi na
sekondari za serikali, imeweza kuunganisha mawasiliano kwa ofisi za
serikali kuanzia ofisi za wilaya, vituo vya polisi na ofisi za posta
kuwawezesha kufanya kazi zao kwa ufasaha” alisema Bwana Trung
Halotel
ni mtandao wa kwanza kupeleka mawasiliano kwa vijiji elfu nne (4,000)
ambavyo havikuwa na mawasiliano toka Tanzania kupata uhuru ambapo
matokeo yake imesisimua maendeleo ya wakazi wa vijiji hivyo.alisema
naibu Mkurugenzi huyo.
Kama
wawekezaji wengine Halotel imekuwa mstari wa mbele kwa kusaidia jamii
kufikia maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya kiafya, elimu,
mawasiliano, michezo, kilimo na watu wenye uhitaji maalumu kwenye jamii
zetu.
‘Pia
tunafurahia kuona watanzania hivi sasa wameshika nafasi kubwa za
uongozi (menejiment) makao makuu na katika matawi yetu ya nchi nzima.
Haya ni mafanikio makubwa kuona Halotel inaendeshwa na kusimamiwa na
watanzania na sasa ni wasaa wao wa kuonesha uwezo na maarifa yao kuleta
huduma bora zaidi’. Alisema Trung
Katika
kusheherekea miaka mitano, Halotel imezindua ofa maalum
zitakazowawezesha watanzania kuwasaliana kwa punguzo kubwa. Hii ni mara
ya kwanza kwa Halotel kutoa ofa kubwa kwa wateja wake na ofa hizo
zinajulikana kama, “DABO BANDO” na KUONGEA BURE HALOTEL KWENDA HALOTEL
pia kwa wateja wetu watakua wakipata zawadi mbalimbali ikiwemo vocha
watakapo tembelea maduka ya halotel yaliyoko nchi nzima ndani ya mwezi
huu.
Tunapenda
kuwapongeza wateja wetu kwa kuchagua mtandao wa Halotel kwa miaka yote
mitano ya utoaji wa huduma za mawasiliano na hivyo tunapenda kutoa ofa
hii kama zawadi kwa wateja wetu. Ambapo ofa maalumu ya DABO BANDO, mteja
wa Halotel atapata mara mbili ya kifurushi cha siku cha muda wa
maongezi au intaneti kuanzia tarehe 15 Octoba mpaka 31octoba 2020.
Kifurushi cha siku kinaweza kuunganishwa kwa kupiga menyu ya Halotel
*148*66# kupitia muda wa maongezi au Halopesa. Kwamfano mteja wa Halotel
akijiunga na kifurushi cha siku cha intaneti cha GB 1 atapata GB 1
nyingine bure”. Alisema Trung
Mbali
na Ofa za Halotel, Trung alizindua ofa maalum ya Halopesa ya
“kurudishiwa asilimia 50 ya makato ya kutuma pesa”, kwa mtandao wa
Halotel na mitandao mingine kwa muda wa siku tatu (3) kuanzia terehe 15
hadi 17 Octoba 2020. Pia wakala na washirika wa Halopesa wataweza kupata
zawadi na hati za shukurani.
Pia
alimalizia kwa kutaarifu umma, kwamba mbali na kutoa huduma bora kwa
gharama nafuu. Halotel wataendelea kuleta huduma zenye tija ambazo
zitakidhi mahitaji ya wateja na hiki ndicho kipaumbele cha kampuni yetu.
Halotel
ni tawi la kampuni ya kivietnam Viettel Group ambayo imeanza kutoa
huduma za mawasiliano nchini tangu Octoba 15,2015 ambayo imeweka mkazo
kuunganisha vijiji ambavyo havikuwa na mawasilia ambapo asilimia
themanini (80%) ya watanzania wanaishi huko.
No comments :
Post a Comment