WAFANYAKAZI
wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar
es Salaam huku wakiwa wameshikilia madafu mikononi
wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar
es Salaam huku wakiwa wameshikilia madafu mikononi
WAFANYAKAZI
wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar
es Salaam huku wakinywa maji ya dafu kama wanavyoonekana
wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar
es Salaam huku wakinywa maji ya dafu kama wanavyoonekana
WAFANYAKAZI
wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar
es Salaam wakiwa wamekaa kwenye jamvi na wengine wamesimama
wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar
es Salaam wakiwa wamekaa kwenye jamvi na wengine wamesimama
WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam
WAFANYAKAZI wa Benki I&M wakikata keki ikiwa ni ishara ya wakisheherekea mwezi wa huduma kwa wateja Jijini Dar es Salaam
Na Mwandishi Wetu,Dar es Salaam
BENKI ya I&M Tanzania imeadhimisha Wiki ya
Huduma kwa Wateja, kwa kutambua mchango muhimu unaotolewa na fanyakazi
wake katika kuwahudumia wateja wao kwa viwango vya juu na kuhakikisha
kuwa wanakuwa wenye furaha wakati wote.
Hafla hiyo ilifanyika maktaba square jijini Dar
es Salaam katika makao makuu ya benki hiyo, ikiambatana na shughuli
mbalimbali kwa wateja kama ishara ya shukrani kwa wateja wanaothaminiwa
na pia wafanyakazi wake ambao wamekuwa wakitekeleza jukumu muhimu la
kutoa huduma bora kwa wateja wakati wote.
Miongoni mwa shughuli za kusherehesha hafla hiyo
na wiki ya huduma kwa wateja zilizofanywa na benki hiyo ni pamoja na
Maofisa wa juu na waandamizi wa benki hiyo akiwamo Afisa Mtendaji Mkuu,
walichukua jukumu la kuhudumia wateja katika matawi mbalimbali kwa siku
ya jana.
Sheherehe hiyo ya wiki nzima ni matokeo ya
kujitolea kwa benki hiyo ya I&M katika kuongeza ushiriki wa
wafanyakazi katika kuunga mkono kaulimbiu ya mwaka huu ya siku hiyo
inayosema kuwa, ‘Timu ya ndoto’.
Mbali na ushiriki wa watendaji wakuu, maafisa
waandamizi katika kufanya jukumu la huduma kwa wateja, pia wafanyakazi
wote wa benki hiyo walipokea barua binafsi za shukurani kwa bidii yao na
kujitolea kwao katika kuleta matokeo chanya na furaha kwa wateja katika
benki hiyo.
Mkuu wa Mauzo ya rejareja wa benki hiyo, Lilian
Mtali alisema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wanataka
onyesha thamani ya watoa huduma kwa wateja.
“Sisi benki ya I&M tunataka kutumia wiki hii
ya huduma kwa wateja kuhakikisha kuwa tunawaonyesha thamani na ukarimu
wateja wetu,lakini pia kuunga mkono na kutambua kazi nzuri na kubwa
inayofanywa na maafisa wa huduma kwa wateja kama dawati namba moja
ambalo ni nembo na kilelezo cha huduma bora za benki.
“Kwani sote tunatambua kuwa dawati la huduma kwa
wateja ndilo limebeba sura na kilelezo cha huduma bora zinazotolewa na
benki, wamekuwa wakaifanyakazi kwa bidi kwani hata pale wateja
wanapokuwa na jazba, wao wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha kuwa
wanakamilisha mahitaji yao na kuwaacha wakiwa na furaha jambo ambalo ni
kipaumbele cha benki,” alisema Lilian.
Wiki ya Huduma kwa Wateja ni maadhimisho ya
umuhimu wa huduma kwa wateja na ya watu ambao wanahudumia na kusaidia
wateja kila siku.
Hafla hiyo huadhimishwa kila mwaka wakati wa
wiki ya kwanza ya Oktoba na wafanyabiashara wote na mashirika
yanayolenga huduma kote ulimwenguni, ambayo hutambua umuhimu wa kutoa
huduma bora kwa wateja.
No comments :
Post a Comment