Mkuu
wa Wilaya ya Ilemela Dkt. Severine Lalika, akizungumza kwenye Semina ya
wastaafu iliyoandaliwa na benki ya CRDB mkoani Mwanza katika ukumbi wa
hoteli ya Gold Crest.
Benki
ya CRDB imeendesha semina ya siku moja kwa wastaafu mkoani Mwanza ikiwa
ni sehemu ya utekelezaji wa mpango maalum wa uwezeshaji kwa wastaafu
ambao ulizinduliwa na benki hiyo mwishoni mwa mwezi Septemba.
Akizungumza katika semina hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dkt. Severine
Lalika aliipongeza Benki ya CRDB kwa kuwawezesha wazee huku akielezea
azma ya serikali ni kuhakikisha inatengeneza maisha bora kwa wastaafu
wote nchini kwa kuwajengea mazingira endelevu ya kujiingizia kipato
''Naipongoeza
Benki ya CRDB kwa kuendelea kuwa wabunifu kwa kuja na wazo hili la
kuwakutanisha wastaafu ili kujadili kwa pamoja fursa zinazopatikana
katika benki hii ukizingatia kundi hili la wateja limekuwa
likisahaulika''amesema Dkt. Lakila.
Aidha
amesema kuwa CRDB imefanya jambo kubwa kwa kufanya semina kwa wastaafu
maana ni kitu kigeni kwa benki ya mikopo kuwakutanisha wastaafu kwa
kujadili pamoja na kuwapa mbinu na ujuzi kwa kunijiendeleza kimaendeleo
kwa kuongeza kipato.
Dkt.
Lakila amewapongeza wastaafu wote walioitikia wito kwa kuja kujifunza
mafunzo masula ya kibenki zitolewazo na Benki ya CRDB imani yangu baada
ya kongamano hili kutakuwa na mabadiliko makubwa katika utunzaji na
uwekaji wa fedha pamoja na masuala ya mikopo.
''Leo
ni siku muhimu kwa Benki ya CRDB kwa kutukusanya hapa hivyo naamini
baada ya mafunzo hayo tutapata elimu jinsi ya kuwekeza na kutunza
masuala ya mikopo katika kuboresha maisha yetu''amesema Dkt. Lakila.
Dkt.
Lakila ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuanzisha na kutekeleza mpango huu
wa uwezeshaji kwa wastaafu wenye lengo la kuleta faraja na kuwasaidia
wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbalimbali ya kimaisha zote
tumekuwa tukiona changamoto hivyo mpango huu utaleta tumaini jipya.
Meneja
wa Uwezeshaji kwa Wateja Benki ya CRDB, Crispin Sichwale akizungumza
juu ya fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa wastaafu katika semina
iliyoandaliwa na benki hiyo mkoani Mwanza.
Kwa
upande wake Meneja wa Benki ya CRDB Uwezeshaji kwa Wateja, Chrispin
Sichwale alisema mpango huo wa uwezeshaji kwa wastaafu anajumuisha fursa
za kujiwekea akiba, uwekezaji, pamoja na uwezeshaji wa kifedha kwa
wastaafu. Sichwale alisema hivi karibuni Benki hiyo imezindua huduma za
akaunti maalum ya wastaafu “Pension Account” na huduma ya uwezeshaji wa
kifedha kwa wastaafu kidijitali “Pension Advance” kupitia huduma ya
SimBanking App, ambapo wastaafu hupata mkopo bure.
“Ninajivunia
kuwajulisha kuwa hadi leo hii tukiwa tunazindua mpango huu wa
uwezeshaji wastafu, tayari wastaafu zaidi ya 19,000 wameshafungua
akaunti hii na wanafurahia huduma zetu,” alisema Sichwale huku
akibainisha kuwa kupitia akaunti hiyo wastaafu wanapewa TemboCard
inayowawezesha kupata huduma kwa CRDB Wakala na ATM zote nchi nzima.
Sichwale
alisema kupitia mpango huo wa uwezeshaji kwa wastaafu benki hiyo pia
imejipanga kuendelea kutoa mikopo kwa wastaafu ili kuwawezesha
kuendeleza biashara na miradi yao ya maendeleo na hivyo kupunguza ukali
wa maisha ya kila siku. Kupitia mkopo huo Wastaafu wanaweza kukopa
kuanzia shilingi milioni 1 hadi shilingi milioni 100 kwa kipindi cha
mwaka 1 hadi 7.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili
No comments :
Post a Comment