Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba,
huduma za kibenki zinazotolewa na benki na taasisi za fedha nchini
zitaendelea kutolewa kama kawaida kwa wateja kabla, wakati na baada ya
Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28, 2020,
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 15, 2020 na Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Kwa
mujibu wa idara hiyo,Benki Kuu inawataka wananchi kupuuza taarifa
potofu zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kwamba kuna maelekezo ya
kusitisha huduma hizo muhimu katika kipindi cha uchaguzi.
"Benki
Kuu ya Tanzania, kama msimamizi wa benki na taasisi za fedha, haijatoa
maelekezo yoyote ya kusitisha huduma za kibenki kwa wateja wa taasisi
hizo. Wananchi wataendelea kupata huduma zote za kibenki kama kawaida
wakati wote kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi.
"Aidha,
Benki Kuu inapenda kutoa onyo kwa mtu, watu au kikundi cha watu wenye
dhamira ya kupotosha umma na kusababisha taharuki katika jamii kwa kutoa
taarifa za uongo. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu,
watu au kikundi chochote kitakachobainika kutoa taarifa potofu kwa
umma,"imebainisha sehemu ya taarifa ya Idara ya Uhusiano wa Umma na
Itifaki ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
No comments :
Post a Comment