Ndege aina ya Airbus
A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132, ikituwa kwa mara ya kwanza
katika Uwanja wa ndege wa Dodoma baada kufanyiwa marekebisho kwa
kupanuliwa kwa njia ya kutua na kufikia urefu wa kilometa 2.8.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Bilinithi Mahenge,akizungumza mara baada ya kuipokea
Ndege aina ya Airbus
A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132,ambayo imetuwa kwa mara ya
kwanza katika Uwanja wa ndege wa Dodoma baada kufanyiwa marekebisho kwa
kupanuliwa kwa njia ya kutua na kufikia urefu wa kilometa 2.8.
Mkurugenzi Mkuu wa
Wakala wa Barabara nchini(TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale,akitoa
taarifa mara baada ya kuipokea Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye
uwezo wa kubeba abiria 132, ikituwa kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa
ndege wa Dodoma baada kufanyiwa marekebisho kwa kupanuliwa kwa njia ya
kutua na kufikia urefu wa kilometa 2.8.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk.Leonard Chamuriho,akizungumza
mara baada ya kuipokea Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa
kubeba abiria 132, ikituwa kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa ndege wa
Dodoma baada kufanyiwa marekebisho kwa kupanuliwa kwa njia ya kutua na
kufikia urefu wa kilometa 2.8.
Abiria wakishukwa kwa
mara ya kwanza wakiwa na Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa
kubeba abiria 132,baada ya kutua katika Uwanja wa ndege wa Dodoma.
Baadhi ya wakazi wa
Dodoma wakishuhudia Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa
kubeba abiria 132, ikituwa kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa ndege wa
Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Dkt.Bilinithi Mahenge akiwa katika picha mbalimbali mara baada ya
kuipokea Ndege aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132
baada ya kutua kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Dodoma
………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mambo yamezidi kunoga
huku shwange na mafuriko ya wakazi wa Dodoma baada ya kuiona Ndege
aina ya Airbus A220-300 yenye uwezo wa kubeba abiria 132,kwa mara ya
kwanza ikituwa katika Uwanja wa ndege wa Dodoma baada kufanyiwa
marekebisho makubwa kwa kupanuliwa kwa njia ya kutua na kufikia urefu wa
kilometa 2.8.
Ndege hiyo imetua
jijini Dodoma na kupokelewa na viongozi mbalimbali,wananchi huku
wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Bilinithi Mahenge.
Baada ya kupokea
ndege hiyo, Dk.Mahenge amesema kuwa kutua kwa ndege hiyo inatokkana na
Juhudi za Rais Dkt.John Magufuli kwa kuleta maendeleo kwa watanzania
ili kurahisisha huduma za usafiri wa anga.
Hivyo Serikali
imeamua kuboresha miundombinu ya huduma za usafiri wa ndege katika jiji
la Dodoma ambao utawasaidia wakazi wa Dodoma kuachana na gharama kubwa
za usafiri walizokuwa wakitumia awali kabla ya kuboreshwa kwa huduma za
usafiri.
“Uwapo wa ndege hii
ni mkubwa itakuwa inabeba abiria 132 kwani hapa zamani tulikuwa na ndege
ambayo ilikuwa inabeba abiria 12 na bei yake ilikuwa ni Sh.530,000
wakati hii bei unaenda Dar es Salaam na kurudi ,”amesema Dkt.Mahenge
Kwa kweli nipende
kusema kuwa kazi kubwa imefanywa na Rais Dkt,Magufuli kwa kuwajali watu
wa kila aina kwa kuwaleta maendeleo kwa haraka lazima tumpongeze kwa
hilo maana wana Dodoma ametushibisha tuendelee kumsaidia ili azidi
kuing’arisha nchini yetu.
Naye Mkurugenzi Mkuu
wa Wakala wa Barabara nchini(TANROAD), Mhandisi Patrick Mfugale, amesema
kuwa uwanja huo awali ulikuwa na urefu wa kilometa 2.5 lakini kwasasa
una kilometa 2.8 hivyo ndege zenye ukubwa wa ndege hii iliyotuwa
zitakuwa zinatua jijini hapa.
Kwa upande wa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk.Leonard
Chamuriho, amesema kuwa uwanja huo ulipanuliwa kwa awamu mbili ya kwanza
ilikuwa kutua kwa ndege ya Bombadier yenye uwezo wa kubeba abiria 76 na
hatua ya pili ni hatua ya kupanua ili ndege yenye uwezo wa kubeba
abiria 132.
No comments :
Post a Comment