
………………………………………………………………………………………
Na.WAMJW-Manyara
Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatambua upungufu
uliopo wa wauguzi kwenye hospitali za rufaa za mikoa nchini na hivyo
kuweka kama kipaumbele kwenye ajira Serikalini.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka wizara ya
afya Bi. Ziada Sellah wakati akiongea na wauguzi na wakunga kwenye
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara.
“Tayari wizara inatambua upungufu huo na kwamba ajira zitakapotoka vipaumbele vitakuwa ni kuongeza waguzi hospitalini
hapo” Alisema Bi. Ziada.
Licha
ya upungufu wa wauguzi katika hospitali hiyo Mkurugenzi huyo pia
amewataka wauguzi hospitalini hapo kuzingatia maadili ya kazi na
kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wagonjwa, ili wagonjwa waweze
kupata ahueni kwa kupatiwa huduma nzuri kutoka kwa wauguzi.
Aliongeza
kuwa kila muuguzi nchini akumbuke kiapo alichokiweka kwa kuzingatia
maadili na miiko ya muuguzi katika kumuhudumia mteja wake
Imetajwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara inakabiliwa na upungufu wa
wauguzi 200. Upungufu huu ni zaidi ya asilimia 60% ya mahitaji.
Mkurugenzi
wa huduma za Uuguzi na Ukunga yupo kwenye ziara ya kikazi ya kukagua
huduma za Uuguzi katika hospitali za Rufaa za mkoa ya
Singida,Manyara,Arusha, Kilimanjaro na Arusha pamoja na hospitali maalum
na kanda ili kusikiliza changamoto zinazoikabili kada hiyo ya wauguzi
na kuzipatia ufumbuzi ili wauguzi waweze kufanya kazi zao katika
mazingira rafiki.
No comments :
Post a Comment