Mwenyekiti
wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Profesa Mayunga Nkunya akizungumza
wakati wa kufunga maonesho ya vyuo vikuu yanayomalizika leo Septemba 5,
katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Septemba.
Maonyesho hayo yakifanyika kwa siku sita ambapo vyuo na wadau mbali
mbali wameshiriki
Katibu
Mtendaji wa TCU , Profesa Charles Kihampa akizungumza wakati wa
kufunga maonesho ya siku sita ya vyuo vikuu yanayomalizika leo Septemba
5, 2020 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Profesa
Mayunga Nkunya akikagua banda la Chuo Kikuu Muhimbili kabla ya kufunga
maonyesho ya 15 ya vyuo vikuu nchini, yanayimalizika leo katika viwanja
vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wadau wa elimu ya wajuu na washirik wa vyuo vikuu wakifuatilia
hotuba ya Profesa Mayunga Nkunya ya kufunga maonyesho ya 15 ya vyuo
vikuu nchini, yanayomalizika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Education Link, Abdullmalik Mollel akizungumza
wakati wa kufunga Maonesho ya vyuo vikuu yanayomalizika leo jijini Dar
es Salaam.
Na Karama Kenyunko Michuzi TV.
TUME
ya vyuo vikuu (TCU), nchini imewataka wale wote wanaotegeme kujiunga na
elimu juu kufanya maamuzi na uchaguzi sahihi wakati wakiomba udahili
kwenye vyuo vya elimu ya juu hapa nchini ili pindi wamalizapo masomo yao
waweze kuhimili soko la ajira.
Pia
vyuo hivyo vya elimu ya juu vimeshauriwa kutoa elimu bora ili kuzalisha
wahitimu mahili, weledi wabunifu na wenye uwezo wa kutatua changamoto
za Jamii, watakaoweza kuhimili ushindani katika soko la ajira kitaifa,
Kikanda na kimataifa.
Mwenyekiti
wa Tume hiyo, Profesa Mayunga Nkunya ameyasema hayo leo Septemba 5,
2020 wakati akifunga maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yaliyokuwa yakifanyika
katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Amesema
serikali imeendelea kuweka kipaumbele maboresho ya elimu nchini na
kupanua wigo na fursa za masomo kwa watanzania na katika ngazi zote za
elimu ikiwemo ya elimu ya juu.
"Natoa
wito kwa Taasisi zote nchini kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali
za kuongeza fursa za masomo kwa Watanzania wengi zaidi lakini bila
kuathiri ubora" amesema Nkunya.
Ameongeza
kuwa, ili kuweza kupata elimu bora inayokidhi mahitaji ya Taifa,
kikanda na Kimataifa Taasisi zote za elimu ya juu zinapaswa kusimamiwa
ili kuhakikisha zinakuwa na mifumo imara ya udhibiti ubora inayolenga
kuzalisha wataalamu wanaohitajia ambapo ili kufikia azma hiyo vyuo
vinahitaji kuwa na viongozi imara, bora, wenye mtazamo chanya, weledi na
wenye maarifa ya kutosha kusimamia sera na miongozo mbali mbali ya
elimu ya juu nchini kwa kuzingatia mabadiriko katika sekta ya elimu ya
juu yanayotokea nchini na duniani kote.
"
Udahili wa elimu ya juu nchini bado uko chini sana.., katika nchi za
Afrika miaka miwili iliyopita udahili ulikuwa kama asilimia nane kwa
wale wanaokidhi vigezo lakini sisi hapa ni asilimia nne tu bado tuko
chini sana... hatuna budi kuongeza bidii ili kuweza kupanua wigo wa
udahili wa wanafunzi katika vyuo vikuu lakini tukizingatia ubora amesema
Profesa Nkunya.
Ameongeza,
hivi karibuni nchi yetu iliingia kwenye orodha ya nchi zenye uchumi wa
kati hayo mafanikio ambayo kila mmoja wetu anapaswa kujivunia, ni hukumu
letu kila.mmojankuchukua hatua.
Pia
Profesa Nkunya ametoa wito kwa viongozi wa vyuo vya elimu ha juu nchini
kusimamia kwa ukaribu na umakini mchakato mzima wa udahili kwa
wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka wa masomo wa 2020, 2021 kwa
kuzingatia miongozo iliyowekwa ili kuondoa usumbufu usiokuwa wa lazima
kwa waombaji, wazazi, walezi wafadhili na wadau wengine wa elimu ya juu.
Kwa
upande wake, Katibu Mtendaji wa TCU, Charles Kihampa amesema katika
maonyeshao hayo ya siku sita, jumla ya Taasisi 67 zimeshiriki ziwemo
taasisi za mafunzo ya ngazi ya elimu ya juu 58, mabaraza ya uthibiti
ubora mawili, wakala na Taasisi nyingine za serikali zilikuwa na bodi
moja ya usajili wa wataalamu. Taasisi za Sayansi techonojia na utafiti
mbili na Taasisi za huduma za kifedha mbili.
Amesema,
malengo ya maonyeshao hayo yalikuwa ni pamoja na kutoa fursa kwa
Taasisi zinazoshiriki kujitangaza kwa kuonesha huduma na kazi mbali
mbali wanazofanya na mchango wao katika ustawi wa elimu ya juu kwa
mustakabali wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia na manufaa yake
kiuchumi na kijamii.
Amesema
pia Maonesho yanawapa fursa wananchi, wafanyabiashara na wenye viwanda
kuweza kujifunza na kuanzisha ushirikiano wa kujenga na kuimarisha
mahusiano baina ya Taasisi hizo za elimu ya juu.
Amesema,
mpaka kufikia leo hii jumla ya wanafunzi 33969 wanaotaka kujiunga na
elimu ya juu wameishatuma maombi yao ya kujiunga na shahada ya kwanza
katika vyuo mbali mbali na pia amewashauri wanaotaka kujiunga katika
degree za awali iuendelea kutuma maombi yao katika dirisha hilo kwanza
ambalo linatarajiwa kufunga Septemba 25, mwaka huu na siyo kusubiri
mpaka wanapokaribia kufika mwisho ndio waanze kuangaika.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdullmalik Mollel
akizungumza kwa niaba ya washiriki, amevushauri vyuo vikuu vya ndani
hapa nchini kuweka viwango vya kumtambua ama kumruhusu mwalimu aajiriwe
kujikita kwenye uwezo wa msingi (competent base) na siyo ufaulu wa GPA.
"Tunaona
sisi vyuo vikuu vya nje, mwalimu anaweza kuwa na GPA ndogo lakini
output ya kijana wake ikawa ni nzuri sana ni vema ukatengenezwa mfumo
ili vyuo vikuu vyetu vya ndani viweze kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi
inayoendana na idadi kubwa pia ya wahadhiri katika vyuo hivyo", amesema
Mollel
Ameongeza,
vyuo vinapowekwa vigezo vya juu sana katika kumdahili mwalimu
inawezekana tukajitengenezea ushindani mkubwa na kutengeneza uhitaji kwa
wale wachache waliopo na vyuo vikashindwa kupanuka kwa haraka.
Mollel
pia amevipongeza vyuo vikuu vyote na Taasisi za elimu ambazo zimefanya
udahili wa moja kwa moja viwanjani hapo kwa kuweza kuwapa wanafunzi
majibu ya moja kwa moja.
No comments :
Post a Comment