Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dt.Ali Mohamed
Shein (kushoto) akisalimiana na viongozi mara baada ya kuwasili katika
viwanja vya Mradi wa Nyumba za Makaazi za "ZSSF MBWENI REAL ESTATE"
zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es
Salaam kwa ajili ya kuzifungua rasmi Septemba 21, 2020. (IKULU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed
Shein (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF, Dkt.Suleiman
Rashid Mohamed alipowasili katika viwanja vya Mradi wa Nyumba za
Makaazi za "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO
CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuzifungua
rasmi Septemba 21,2020. (IKULU).
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa ZSSF,Sabra
Issa Machano alipowasili katika viwanja vya Mradi wa Nyumba za Makaazi
za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuzifungua rasmi
Septemba 21, 2020. (IKULU).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed
Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi
(katikati) wakifuatana na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa ZSSF, Sabra
Issa Machano pamoja na viongozi wengine mara baada ya kukagua nyumba za
Mradi wa Nyumba za Makaazi za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na
kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam
alipofanya ufunguzi rasmi Septemba 21, 2020. (IKULU).
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein
(katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko
wa ZSSF, Sabra Issa Machano (kushoto) mara baada ya kukagua Nyumba za
Mradi wa Nyumba za Makaazi za "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na
kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam
alipofanya ufunguzi rasmi leo,kulia ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Balozi
Mohamed Ramia Abdiwawa. (IKULU).
Baadhi
ya viongozi mbalimbali waliohudhuria katika Ufunguzi wa Mradi wa Nyumba
za Makaazi za "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO
CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam, zilizofunguliwana Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein
(hayupo pichani) Septemba 21, 2020. (IKULU).
Viongozi
mbalimbali kutoka taasisi za Serikali waliohudhuria katika Ufunguzi wa
Mradi wa Nyumba za makaazi za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na
kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam
zilizofunguliwa Septemba 21, 2020 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).(IKULU).
Baadhi
ya wafanyakazi wa idara mbalimbali za Mfuko wa ZSSF wakiwa katika hafla
ya ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za Makaazi za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE"
zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es
Salaam zilizofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).(IKULU).
“Tuzingatie
kwamba nyumba hizi ni za kisasa, tunahitaji tuzitumie kisasa, shughuli
kama zile za kutwanga, kufuga kuku na nyenginezo itabidi tuangalie
uwezekano wa kuzifanya sehemu nyengine”, alisema.
Amesema nyumba
hizo ni za gharama kubwa, hivyo akaitaka ZSSF kuondokana na muhali
katika ukusanyaji wa fedha ili hatimae ziweze kulipia gharama za ujenzi.
Amewataka wanunuzi wasighafilike kulipa madeni yao ili ZSSF iweze kupata nguvu na kubuni miradi mingine ya maendeleo.
Dkt.Shein
amesitiza umuhimu wa wakazi wa nyumba hizo kuendeleza silka na tamaduni
za maisha ya Kizanzibari kwa kuishi kwa ujirani na mashirkiano.
Aidha,
Rais Dkt.Shein amesema, ujenzi wa nyumba hizo ni mfano mzuri wa namna
Serikali inavyotekeleza dhamira ya matumizi bora ya ardhi iliopo, pamoja
na utekelezaji wa vitendo wa azma ya muasisi wa Mapinduzi matukufu ya
ya Zanzibar ya 1964, marehemu Abeid Amani Karume katika kuwapatia
wananchi makaazi bora, ingawaje wametumia fedha zao.
Amesema,
marehemu mzee Karume alianza na ujenzi wa nyumba za kisasa katika maeneo
mbali mbali Unguja na Pemba, ikiwemo Kikwajuni, Kilimani, Michenzani,
Gamba, Makunduchi na Bambi (kwa Unguja), pamoja na Chakechake, Mkoani,
Kengeja na Wete kisiwani Pemba, kwa kutambua kuwa makaazi bora ni
miongoni mwa mahitaji ya msingi katika maisha ya binadamu.
Baadhi
ya wafanyakazi wa idara mbalimbali za Mfuko wa ZSSF wakiwa katika hafla
ya ufunguzi wa Mradi wa Nyumba za Makaazi za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE"
zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es
Salaam zilizofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).(IKULU).
Katibu
Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Kiongozi, Dkt.Abdulhamid Yahya
Mzee (kulia) pamoja na viongozi wengine wakiwa katika hafla ya ufunguzi
wa Mradi wa Nyumba za makaazi za"ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa
na kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam
zilizofunguliwa Septemab 21,2020 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.(IKULU).
Pichani
ni miongoni mwa nyumba za Mradi wa "ZSSF MBWENI REAL ESTATE"
zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es
Salaam zilizofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.(IKULU).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Khamis Mussa Omar alipokuwa
akitoa taarifa ya Kitaalam Ujenzi wa Nyumba za Mradi wa "ZSSF MBWENI
REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING
CONSTRUCTION ya Dar es Salaam kwa mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein na wananchi
wakati wa hafla ya ufunguzi zilizofunguliwa Septemba 21,2020 Mbweni
Magharibi A Unguja. (IKULU)
Waziri
wa Fedha na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa alipokuwa
akimkaribisha mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein kuzungumza na na wananchi wakati wa
hafla ya Ufunguzi wa Nyumba za Mradi wa "ZSSF MBWENI REAL ESTATE"
zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es
Salaam alizozifunguliwa Septemba 21, 2020. (IKULU).
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Ali Mohamed Shein
(katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa nyumba za Mradi
wa "ZSSF MBWENI REAL ESTATE" zilizojengwa na kampuni ya DEZO CIVIL ENGINEERING CONSTRUCTION ya Dar es Salaam alizozifunguliwa Septemba
21,2020. Kulia ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Balozi Mohamed Ramia
Abdiwawa,Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
(kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya ZSSF, Dkt.Suleiman Rashid Mohamed (wa
pili kushoto). (IKULU).
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed
Shein akisoma Jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za ZSSF Mbweni
Real Estate, baada ya kuondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi
wakati wa hafla ya ufunguzi wa nyumba hizo zilizoko katika eneo la
Mbweni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja jijini Zanzibar,kulia kwa Rais ni
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa.
(IKULU).
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Ali Mohamed Shein,
akimsikiliza Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii
Zanzibar (ZSSF),Bi.Sabra Issa Machano, wakati akitembelea moja ya nyumba
hizo baada ya kuzifungua rasmi Septemba 21,2020 na kushoto kwa Rais ni
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi. (IKULU).
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Khamis Mussa akizungumza na kutoa
maelezo ya kitaalam ya Mradi wa Ujenzi wa Nyumba za ZSSF Mbweni Real
Estate Zanzibar, wakati wa ufunguzi wa nyumba hizo zilizopo katika eneo
la Mbweni jijini Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Ali Mohamed
Shein, akimkabidhi ufungo mmoja wa wanunuzi wa nyumba hizo, Hamid Khamis
Othman wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa mradi huo uliofanyika katika
viwanja nyumba hizo Mbweni jijini Zanzibar.(IKULU).
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed
Shein, akimkabidhi fungo za moja ya nyumba hizo mnunuzi, Talib Mfaume
Hassan, wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa nyumba hizo uliofanyika
Mbweni jijini Zanzibar.(IKULU).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed
Shein amewataka wanunuzi wa nyumba katika eneo la mradi wa nyumba za
makazi Mbweni, kuheshimu sheria za ujenzi wa nyumba hizo na kuzingatia
ramani,anaripoti Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar.
Dkt.Shein ametoa
kauli hiyo katika hafla ya ufunguzi wa mradi wa nyumba za maakazi ‘ZSSF
Mbweni Real estate’, iliyofanyika eneo la Mbweni, nje kidogo ya Jiji la
Zanzibar.
Amesema, kuna umuhimu kwa wanunuzi wa nyumba hizo
kuheshimu sheria za ujenzi unaozingatia ramani halisi na hivyo kuepuka
hatua zozozte za kuzifanyia mabadiliko ya muundo au kuzipaka rangi,
kinyume na taratibu.
Amesema sio jambo la busara kwa wananchi
wanaonunua nyumba hizo bila ya kujali ramani halisi ya ujenzi wakaanza
kuzifanyia mabadilko kwa kuzingatia kuwa nyumba hizo ni za kisasa,
sambamba na kusisitiza matumizi bora na taratibu njema za kuishi ,
zinazoepusha ufugaji wa aina mbali mbali za mifugo.
Ameeleza kuwa, Serikali ya Awamu
ya Saba, kama zilivyo awamu zilizotangulia, zimekuwa zikitekeleza juhudi
za kuimarisha makaazi ya wananchi, ikiwemo eneo hilo la Mbweni
alilosema lina historia kubwa katika nchi.
Alitoa shukurani kwa
ZSSF kwa kufanikisha ujenzi huo na kubainisha matumaini yake kuwa hatua
ya kuwekeza miradi ya namna hiyo itasukuma mbele maendeleo ya nchi kwa
kuinufaisha jamii pamoja na kuleta haiba nzuri ya miji.
“Hongereni
ZSSF na uongozi wote wa Wizara Fedha na Mipango, ZSSF inafanya kwa
vitendo kuinua mazingira ya wananchi Unguja na Pemba katika Nyanja mbali
mbali ikiwemo ya makazi na michezo”, alisema.
Aidha, Dkt. Shein
alibainisha kuwa maendeleo ya nchi yoyote ile huonekana kutokana na
ujenzi wa majengo na kusema ujenzi wa majengo ya kisasa katika maeneo
mbali mbali ya nchi yanatoa taswira ya maendeleo hayo.
Katika
hatua nyingine, Dkt. Shein aliitaka ZSSF kuhakikisha kunakuwepo ulinzi
katika neo hilo ili kudumisha amani kwa wakaazi wake,na kusema jambo
hilo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Vile vile,
aliitaka ZSSF kuhamasiha upandaji ya miti ya vivuli katika eneo hilo,
kuharakisha ujenzi wa majengo yaliobaki katika mradi huo pamoja na
kuvutia wafanyabiashara ili kuanzisha miradi mbali mbali ya utoaji
huduma, kama vile kumbi za mikutano na ujenzi wa skuli.
Alitoa
shukurani kwa taasisi na watu wote walioshiriki katika utekelezaji wa
mradi huo , akiwemo mkandarasi wa mradi ‘Dezo Civil Contactors’.
Mapema,
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa
alitoa shukrani kwa Dk. Shein kwa kuitia moyo ZSSF na kufanikisha
ujenzi hu na kulifanya eneo hilo kubadilika na kuwa mji mdogo.
Alitoa
wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika nyanja tofauti za utoaji wa
huduma ikiwemo ujenzi wa maduka ili kuwaondolea usumbufu wakaazi wa eneo
hilo kufuata huduma hizo masafa ya mbali.
Aidha, aliishukuru
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kusimamaia utekelezaji wa sera ya
Taifa katika makaazi, na kubainisha faida mbali mbali zinazotokana na
mradi huo ikiwemo za kiuchumi na kijamii.
Nae, Katibu Mkuu Wizara
ya Fedha Mipango. Khamis Mussa Omar, alisema mradi wa Nyumba za Makaazi
eneo la Mbweni, unaohusisha majengo 15 na vyumba 210, unafanyika
kupitia Kampuni ya Kizalendo ya ‘Dezo Civil Contractors’ na pale
utakapokamilika utagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 35.
Aliipongeza
Serikali kwa kuipatia ZSSF eneo la ziada kwa ajili ya uendelezaji wa
miradi yake pamoja na kuupongeza Uongozi uliopita wa taasisi hiyo kwa
kuasisi kazi za uwekezaji na uendelezaji wa eneo hilo.Amesema, ujenzi
huo utachochea maendeleo na kuimarisha haiba ya nchi.
Katika
hafla hiyo ambapo viongozi mbalimbali wa serikali walishiriki, akiwemo
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein
alipata fursa ya kukabidhi funguo na hati za nyumba kwa baadhi ya
wamiliki wa nyumba hizo.
No comments :
Post a Comment