Saturday, September 26, 2020

Umuhimu wa elimu ya uwekezaji wa pensheni kwa wastaafu

Most Americans Have Less Than $1,000 in Savings – The Premier Online  Magazine for Black Men

Mstaafu akiwa na mkewe wakifurahia matunda ya kuwekeza pensheni baada ya kustaafu.

Na Christian Gaya

Majira Ijumaa 25 Septemba.2020

Utafiti uliofanywa hivi karibuni unaonesha ya kwamba zaidi ya asilimia 40 ya Watanzania hawajawahi kusikia kuhusu hisa, vipande na hatifungani za muda mfupi wala hatifungani za muda mrefu, huku idadi ya wanawake ikiwa ni kubwa zaidi ikiiongoza kuliko idadi ya wanaume.

Hii inamaanisha kuwa elimu zaidi kuhusu uwekezaji kwenye dhamana za serikali, pensheni na fedha inahitajika sana kwa wananchi.

Hivyo kuna haja kubwa ya kujua faida ya kuwa na akiba kwa Watanzania, na jinsi ya kutenga na kulimbikiza pensheni au fedha ikiwemo na maana ya uwekezaji pamoja.

Pia kuna haja kujua vigezo muhimu vya kuzingatia kabla ya kutoa na kuiweka pensheni yako katika biashara au kitega uchumi chochote kama hisa, vipande, hatifungani na changamoto zake mbalimbali zinazoathiri uwekezaji kama vile mfumuko wa bei.

Kwa kawaida mfumuko wa bei hupimwa kwa kuangalia fahirisi ya bei kitaifa katika kapu la bidhaa na huduma mbalimbali za jamii kwa kipindi fulani kwa mfano mwaka mmoja au hata mwezi mmoja. Mfumuko wa bei huathiri thamani kama vile thamani ya pensheni ya mstaafu.

Kama mfumuko wa bei utakuwa mkubwa sana basi itapunguza kwa kiwango kikubwa thamani ya pensheni na thamani ya hisa na hatimaye kuwakatisha tamaa wawekezaji wa muda mrefu wakiwemo hata wastaafu.

Lakini iwapo mfumuko wa bei na viwango vya riba vitathibitiwa basi wawekezaji kama vile wastaafu na watu mbalimbali watahamasika kuwekeza zaidi katika hisa.

Viwango vya riba vinavyotolewa na serikali hasa kwenye hatifungani za serikali yaani dhamana za serikali vinaweza kuathiri bei za hisa iwapo riba zitakazotolewa zitakuwa kubwa sana.

Kwa mfano, wastani wa asilimia 15 mpaka 20 wakati faida au marejesho ya gawio kwa hisa ni la wastani wa asilimia 10-15, basi wawekezaji watawekeza zaidi kwenye dhamana za serikali kuliko hisa na hii itasababisha soko la hisa kukosa wanunuzi na kuwa na wauzaji zaidi na kusababisha kuporomoka kwa bei ya hisa.

Mstaafu akitaka kununua baadaye anaweza kuuza hisa zake na kupata fedha. Kuna uwezekano kuwa wakati mstaafu akitaka kuitumia fedha hiyo haitamwezesha kununua idadi ya mahitaji yake kama ambavyo angeitumia leo. Hii inatokana na kupungua kwa thamani ya fedha kwa sababu ya mfumuko wa bei.

Mfumuko mkubwa wa bei huathiri zaidi hatifungani zenye riba maalumu isiyoongezeka kuliko hisa. Unafikiri kwa nini inakuwa hivyo? Kwa sababu hatifungani za muda mfupi au mrefu haziongezeki thamani lakini hisa zina uwezo wa kukua kwa thamani.

Ili mstaafu aweze kupambana na mfumuko wa bei, ni bora akawekeza katika hisa, vipande, amana za serikali au kwenye hatifungani zenye kutoa faida kubwa kuliko mfumuko wa bei ili kumwezesha mstaafu mwekezaji kutopoteza thamani ya fedha aliyowekeza.

Kwa mfano, kama mfumuko wa bei ni asilimia 8, basi kama mstaafu mwekezaji anatakiwa kuhakikisha angalau anapata kuanzia faida ya asilimia 10 na kuendelea kwa kila shilingi uliyowekeza.

Iwapo watu hatakuwa na fedha kwa sababu mbalimbali yaani kukosa wanunuzi kutokana na ukwasi, hii itasababisha wastaafu wawekezaji wengi kuuza hisa zao ili wapate fedha na hivyo inaweza kusababisha kushuka kwa bei ya hisa.

Kwa upande mwingine ni juu la suala la hasara ni kwamba mstaafu mwekezaji makini hatakubali kumiliki hisa kwa kuwa alishawekeza fedha hapo.

Kuna wakati madalali huwa wanakosea kwa bahati mbaya na kuuza hisa nyingi zaidi ya alizoagiziwa. Hisa zilizozidi oda za mauzo kama zikiwa chache.

Wateja wa hizo hisa mara nyingi huwa wanaagizwa ya kwamba asirekebishe, ila hupelekewa cheti cha hisa na kumpatia oda mpya itakayowiana na idadi ya hisa chache alizouza kimakosa. Isipokuwa hapo ni pale ambapo huyo mtu alikuwa mwaminifu ingawa alikuwa amekosea.

Lakini kwa upande mwingine kuna madalali wengine wasio waaminifu hata kidogo ambao hupelekea kuuza bila ridhaa ya mwanahisa kwa kujua kabisa au kufanya hivyo kwa makusudi.

Kosa kama hili la kukosa uaminifu hutokea wakati ule hisa zinapouzwa na dalali bila kibali cha mwanahisa au oda ya mwanahisa, kwa bei kubwa sasa, huku akitarajia bei kushuka siku sijazo, na kupata fursa ya kununua tena hisa zile zile kwa bei nafuu zaidi, huku akiweka mfukoni faida kati ya bei kubwa aliyouza na bei ndogo aliyonunua. Ni aina ya uviziaji uliochanganyika na kukosekana kwa uaminifu.

Hitilafu ni kuchukua dhamana yaani hisa au vipande vya mtu au kampuni bila mmiliki kujua, pia bila idhini ya mmiliki na kuziuza kwa bei kubwa akitarajia ya kuwa bei itakuja kushuka siku zijazo ili aje anunue na kuja kufidia. Ambalo ni jambo la kujikopesha bila idhini ya mwanahisa.

Mara nyingi mtu atendaye jambo kama hili husubiri bei inaposhuka, na hununua tena hisa zile zile kwa jina la mmiliki wa mwanzo na kurudisha ule mkopo wa hisa kinyemele.

Lakini ikiwa bei haitashuka kama ilivyotarajiwa, basi mhusika hupata hasara kwa kuwa itambidi anunue hisa zile zile kwa bei kubwa ili afidie mkopo au deni la hisa alizojikopesha ambalo ni kosa la jinai.

Mwanahisa hawezi kukugundua kirahisi kwa kuwa jumla ya idadi ya hisa zake zinabaki kuwa zile zile labda apate taarifa ya akaunti yake ya hisa na kuhoji.

Hata kama ukihoji, makosa yanaweza kutokea na usijue tofauti kati ya kosa na hujuma. Soko la hisa la Nairobi (NSE) hutumia wanahisa wake taarifa ya akaunti ya hisa kila panapokuwa na mabadiliko.

Iwapo dalali atauza hisa na baadaye bei ikapanda badala ya kushuka, basi atapata hasara kama akifidia. Lakini kama ni hisa nyingi, anaweza akashidwa kulipia ongezeko la bei na kuwa hasara ya kudumu kwa mwanahisa. Mamlaka inayohusika inatakiwa kuchukua hatua za kinidhamu kwa watendaji na wadau wasio waaaminifu.

Ili kulinda maslahi ya wastaafu na wadau wengine wa soko la hisa yaani wanunuzi, wauzaji, madalali na wengineo, sheria zimetugwa na mamlaka mbalimbali zimeanzishwa. Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Msajiri wa Makampuni (BRELA), Soko la Hisa la Dar Es Salaam (DSE) na mamlaka nyinginezo ni baadhi ya sheria na mamlaka zinazohusika kutoa usimamizi wa kisheria na mwongozo wa masoko ya dhamana yaani hisa na hatifungani.

No comments :

Post a Comment